Home BUSINESS SEKTA YA MADINI KUFUNGAMANISHWA NA SEKTA NYINGINE ZA KIUCHUMI

SEKTA YA MADINI KUFUNGAMANISHWA NA SEKTA NYINGINE ZA KIUCHUMI

GST fanyeni Kazi kwa ushirikiano: Mavunde

Waziri Mavunde aja na Vision2030 Madini ni Maisha na Utajiri

Imeelezwa kuwa, Sekta ya Madini inapaswa kufungamanishwa na Sekta nyingine ikiwemo Sekta ya Kilimo, Maji, Nishati, Ujenzi, Viwanda na Biashara ili kuleta tija na maendeleo kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunda wakati akifunga kikao kazi cha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kilichofanyika leo Septemba 17, 2023 katika ukumbi wa Magadu uliopo mkoani Morogoro.

Amesema Tanzania imegawanywa katika QDS 322 Kila moja ikiwa na eneo la kilomita za mraba 2916 ambapo utafiti wa kina wa jiofizikia kwa njia ya kurusha ndege umefanyika kwenye baadhi ya maeneo kwa asilimia 16 tu, Utafiti wa Jiolojia umefanyika kwa asilimia 97 na Utafiti wa jiokemia umefanyika kwa asilimia 24.

Aidha, Mavunde amesema Wizara imeanza kuainisha Dira ya 2023 inayojulikana kama “Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri” ambayo utekelezaji wake utategemea uwepo wa taarifa za tafiti za jiosayansi zinazoonesha uwepo, ubora uwingi wa rasilimali madini.

Hivyo, katika kufikia dira hiyo ya 2030, pamoja na Mambo mengine, GST inatakiwa kufungamanisha Sekta ya Madini na sekta nyingine kukamilisha kufanya utafiti wa jiolojia kwa eneo lote la nchi ili kuhakikisha kuwa kuna taarifa zote za jiolojia za eneo lote la nchi. Aliongeza kuwa taarifa hizo sio muhimu tu kwa maendeleo ya Sekta ya Madini bali pia kwa ukuaji wa Sekta ngingine za kiuchumi kama Maji, Kilimo, Nishati, Ujenzi na n.k.

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga amewataka watumishi wa GST kufanya kazi kwa ushirikiano na ubunifu ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Naye, Mtedaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba amesema lengo la Kikao Kazi ni hicho ilikuwa kujadili muelekeo na kuweka mikakati ya utekelezaji wa Taasisi hiyo kufuatia Kikao Kazi cha Watendaji na Wenyekiviti wa Bodi za Mashirika ya Umma kilichoitishwa na Msajili wa Hazina.

Katika hatua nyingine, Dkt. Budeba amesema ili kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na maelekezo Vision 2030, GST imekuja na maazimio ya kuanza na kuendelea na Mpango kazi uliokwisha andaliwa wa utekelezaji wa tafiti za jiofizikia, jiokemia na jiolojia kwa kuzingatia umuhimu wa madini yakiwemo Madini Adimu na Mkakati.

Previous articleGST YATAKIWA KUWA KINARA WA TAARIFA ZA MADINI NA HUDUMA BORA ZA MAABARA
Next articleDHANA YA MAGEUZI NI UWANJA MPANA – OTHMAN
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here