Home BUSINESS GST YATAKIWA KUWA KINARA WA TAARIFA ZA MADINI NA HUDUMA BORA ZA...

GST YATAKIWA KUWA KINARA WA TAARIFA ZA MADINI NA HUDUMA BORA ZA MAABARA

Kupitia utekelezaji wa muelekeo mpya ujulikanao kama Vision 2030, Serikali yaweka mkakati wa kuifanya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) kuwa kinara wa upatikanaji na utoaji wa taarifa za madini na pia huduma bora za maabara.

Hayo yamesemwa leo tarehe 17 Septemba, 2023 Mkoani Morogoro na Waziri wa Madini, Mh. Anthony MavundeĀ  alipokuwa akifunga kikao kazi cha Menejimenti ya GST ambacho kilikuwa mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan wakati akizungumza na wakuu wa Taasisi za umma Jijini Arusha na kupitia muelekeo mpya wa Wizara wa VISION 2030: Madini ni Maisha na Utajiri

ā€œNchi yetu imegawanywa katika QDS 322, ambapo QDS moja ina eneo la kilometa za mraba 2916. Ni asilimia 16 pekee ya eneo lote nchini ndilo limefanyiwa utafiti wa jiofizikia kwa teknolojia ya kisasa ya kurusha ndege yaani High Resolution Airborne Geophysical Survey.

Sote tunaona kwamba iwapo tukiweza kufanya utafiti wa eneo hata kwa asilimia 50 tu, namna ambavyo sekta ya madini inakwenda kulinufaisha Taifa letu kwa kuchangia zaidi kwenye ukuaji wa uchumi.

Mh. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan , ameonesha dhamira ya dhati ya kuikuza sekta ya madini ili iongeze mchango zaidi kwenye Pato la Taifa la Nchi yetu.

Taasisi hii inategemewa kwa taarifa za awali za muelekeo wa miamba, hivyo tunakwenda kuifanya kuwa kinara wa taarifa na takwimu za madini nchini,sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wake ili kukidhi mahitaji ya dunia ya leo na pia kuimarisha maabara yake kwa vifaa vya kisasaā€Alisema Mavunde.

Awali, akitoa maelezo ya utangulizi, Afisa Mtendaji Mkuu wa GST, Dkt. Mussa Budeba alieleza kuwa kikao kazi hicho ni matokeo ya Mkutano wa Mhe. Rais alipokutana na Wenyeviti na Watendaji wa Taasisi za Serikali ambapo alielekeza Taasisi zijiwekee mikakati ya kujiendesha kwa tija na faida na kupunguza utegemezi kutoka Serikalini.

Vilevile, mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye ni Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga alibainisha kwamba pamoja na masuala mengine kikao kazi hicho kililenga pia kuongeza ari ya kazi, ushirikiano baina ya watumishi kwa kufanya kazi kwenye Timu ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mh. Rebecca Nsemwa alishukuru kwa GST kuchagua kufanyia kikao Morogoro na kuiomba GST kuuweka Mkoa wa Morogoro kwenye mkakati wao kwani wanao utajiri mkubwa wa madini.

Previous articleSERIKALI KUTUMIA MIEZI 18 KUMALIZA ADHA YA UMEME MASASI
Next articleSEKTA YA MADINI KUFUNGAMANISHWA NA SEKTA NYINGINE ZA KIUCHUMI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here