Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan jiwe la msingi ujenzi wa Halmashauri ya Mtama na kusalimia wananchi wa Mtama leo tarehe 18 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kilimahewa Ruangwa Mkoani Lindi tarehe 18 Septemba, 2023.
Akina Mama wa Kabila la Wamwera wakiwa wamelala chini kama ishara ya Heshima kubwa ya mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Kilimahewa Ruangwa Mkoani Lindi tarehe 18 Septemba, 2023.
Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Lindi Mhe. Teckla Ungele akicheza pamoja na Akina Mama wa Kabila wa Wamwera wakati wa shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ruangwa Mkoani Lindi tarehe 18 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kilimahewa, Ruangwa Mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 18 Septemba, 2023.
Shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kilimahewa Ruangwa Mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 18 Septemba, 2023.