Home LOCAL RAIS DKT. SAMIA ATEULIWA  MJUMBE WA BODI YA USHAURI YA KITUO CHA...

RAIS DKT. SAMIA ATEULIWA  MJUMBE WA BODI YA USHAURI YA KITUO CHA DUNIA CHA UHIMILIVU WA MABADILIKO YA TABIANCHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteuliwa rasmi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia cha Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi (Advisory Board of the Global Centre on Adaptation – GCA).

Taarifa ya uteuzi huo iliwasilishwa na Mhe. Ban Ki-moon, Mwenyekiti wa Bodi ya GCA na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa alipokutana na Mhe. Rais pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Nairobi, Kenya.

Heshima hii ni utambuzi wa uongozi mahiri wa Rais Samia katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Afrika na duniani kote ambapo Tanzania ni kinara kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali barani Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here