Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud amesitisha Leseni ya nyumba moja ya kulala Wageni iitwayo Nice Beach Resort iliyopo Kidimbwi mkoani humo, kwa Madai ya kufanya kazi zake kinyume na sheria Zanzibar.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa kuamkia Septemba 5,2023 katika nyumba hiyo nakukuta kasoro kadhaa ikiwemo Uuzwaji wa vileo bila leseni, pamoja na kuitilia wasiwasi huenda ikawa kunafanyika shughuli za ukahaba ndani ya nyumba hiyo.
Ayoub Mohd Mahmoud pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja amesema, nyumba hiyo ya Nice Beach Resort Haina leseni ya uuzaji wa vileo lakini Cha kushangaza imekuwa ikifanya biashara hiyo kama kawaida jambo ambalo ni kosa kisheria.
Pia amesema hata daftati la kuandikisha majina ya Wageni wanaoingia na kutoka pia halimo.
“Leseni niliyopewa nakala (copy) na Sheha wangu (mwenyekiti wa Kijiji) ni ya Biashara ambayo ni ya Mwaka 2022. Leseni niliyoiona kwako hapa ni Leseni ya kulaza Wageni uliyopewa na kamisheni ya Utalii ya mwaka 2023, hiyo nimeiheshimu na ndo Maana sijaigusa nimeacha. Nilichozuia hapa ni kutouza vileo, na kutopiga muziki kuanzia leo” Alisema RC Ayoub.
Kwa upande wake mmiliki wa Nyumba hiyo Bwan Ali Salum Ali akizungumza Kwa njia ya simu na Mkuu huyo wa Mkoa Kwakuwa hakuwepo hapo bali alimuweka msaidizi wake, alisema leseni za kuuza vileo anayo, Huku akiomba kukutana na RC Ayoub kwa mazungumzo zaidi.
Ombi la mmiliki huyo la kuomba kukutana na RC Ayoub ni kutokana na Mkuu huyo kutompa nafasi ya kumsikiliza Kwa muda huo Huku akisema “nitakupa namba ya Katibu wangu, yeye ndo atakayekupangia lini na saa ngapi uje ofisini” Alisema.
Itakumbukwa kwamba Hatua ya RC Ayoub kuifungia nyumba ya Nice Resort imekuja kutokana na malalamiko ya Wananchi wanaoishi Karibu na maeneo hayo kudai kwamba kuna ukiukwaji Mkubwa wa sheria, Mila na utamaduni wa Zanzibar ambao unafanywa ndani ya nyumba hiyo huku wakitaka Serikali ya Mkoa kuingilia kati jambo Hilo.