Home BUSINESS MAJALIWA KUZINDUA RASMI MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUSAIDIA WAWEKEZAJI

MAJALIWA KUZINDUA RASMI MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUSAIDIA WAWEKEZAJI

Picha ya Maktaba 

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua rasmi mfumo wa kielektoniki utakaowezesha utoaji huduma kwa mara moja kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Septemba 11, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Idara ya Uhamasishaji na Uwekezaji wa TIC John Mnali amesema kuwa uzinduzi huo, ni hatua kubwa iliyofikiwa na TIC katika kuhakikisha wawekezaji wanapata huduma Bora.

Aidha ameongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na maboresho yanayoendelea kufanywa na TIC ili kurahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji na kumaliza changamoto zilikuwepo katika kusajili miradi ya uwekezaji.

“Mfumo buu unaitwa ‘Tanzania Electronic Investment Window’ ambao umetokana na kuunganishwa kwa mifumo ya Taasisi mbalimbali za serikali inayoshughulika na utoaji vibali na leseni kwa wawekezaji wetu.”

“Mfumo huu kwa awamu ya kwanza unaunganisha Taasisi saba ambazo tunaanza na Brela, kwenye usajili wa Kampuni, lakini pia kwa upande wa TRA kwaajili ya TIN (Namba ya Mlipa kodi) pamoja na VAT.

Kwa upande wa TIC  tunashughulika na cheti cha uwekezaji, kwa upande wa Kamishna wa kazi kwaajili ya vibali vya kazi, upande wa uhamiaji kwaajili ya hati za ukaazi kwa wawekezaji wanaomiliki miradi ya uwekezaji, pamoja na wafanyakazi wanaotoka nje ya nchi.  Pia, wapo NIDA kwaajili ya kushughulikia usajili wa vitambulisho, na upande wa ardhi kwaajili ya ardhi.” Amesema Mnali.

Sambamba na hilo, Mnali ameongeza kuwa TIC inatarajia kuzindua mwongozo utaotumika kwa watoa huduma kwa wawekezaji ambao wamekuwa wakisaidia wawekezaji kupata huduma na kuanzisha miradi ya uwekezaji hapa nchini wakiwa nje ya nchi.

“Kuna wawekezaji wengine wako nje ya nchi, wanapohitaji huduma hizi za kuweza, kusaidiwa kupata leseni na vibali mbalimbali. Kazi hii inafanywa na kampuni za ndani lakini kwa kipindi kirefu tumekuwa hatuna mwongozo wa kuweza kuwaongoza wale watu wanaotoa huduma hii” Ameongeza

Mwongozo huo ujulikabao  Investor Services Provider Guideline, utakuwa unatumika kwa watoa huduma hao na kuwawezesha kufanya kazi zao katika ubora na ufanisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here