Home BUSINESS GST: MADINI NI MAISHA, UTAJIRI

GST: MADINI NI MAISHA, UTAJIRI

Wataalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wameahidi kwa pamoja kuungana ili kutekeleza dhana ya Vision 2030 ya Madini ni Maisha na Utajiri kwa vitendo ambapo kwa sasa wanategemea kukamilisha zoezi la Utafiti wa Madini Mkakati ya Nikeli katika leseni ya mwekezaji wa Kampuni ya Mineral Access System iliyopo katika Kijiji cha Nanjilinji Wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi.

Wakizungumza katika eneo la utafiti Meneja wa Sehemu ya Jiolojia kutoka GST Maswi Solomon na Mchumi Mkuu GST Osiah Lameck Kajala kwa pamoja wamesema GST imedhamilia kwa dhati kutekeleza Vision 2023 ya Madini ni Maisha na Utajiri wakitolea mfano kufanya tafiti za madini mkakati kwa wadau wa madini kama inavyofanyika kwa madini ya Nikeli katika eneo la Msitu wa Hifadhi uliopo Kijiji cha Nanjilinji Wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi na madini ya Shaba katika Kijiji cha Mbesa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Kufuatia shughuli hizo, timu ya ukaguzi kutoka GST Makao Makuu imekagua shughuli za ugani zinazoendelea kufanywa na wataalumu wa GST katika leseni ya Kampuni ya Mineral Access System

Aidha, Meneja Sehemu ya Jiolojia Maswi Solomon ameipongeza timu hiyo kwa ushirikiano wanaounesha kwenye kutekeleza majukumu yao ya ugani kwa ufanisi na pia, ametoa wito kwao waendelee na ushikrikiano aliouona kwenye eneo lao la kazi.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Wataalumu waliopo katika eneo la Utafiti Mjiolojia Mkuu Yusto Joseph amesema, mpaka sasa timu hiyo imekamilisha Utafiti wa Jiolojia kwa zaidi ya asilimia 96, utafiti wa Jiofizikia kwa zaidi ya asilimia 20 na Utafiti Jiokemia kwa zaidi ya asilimia 66 kwenye eneo lote la mwekezaji lenye ukubwa wa zaidi ya Kilometa za mlaba 220.

Awali, kilifanyika Kikao Kazi cha kupata taarifa za maendeleo ya utafiti unaoendelea katika eneo hilo kilichofanyika Ruangwa mjini kwa kujadili changamoto zilizopo katika shughuli hiyo kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupeana salama za Mtendaji Mkuu wa GST, managementi ya GST na kukumbushana adhima ya Wizara kuhusiana na dhana ya “Madini ni Maisha na utajiri” ambapo changamoto mbalimbali zilielezwa katika Kikao Kazi hicho ambapo baadhi ya changamoto zilioatiwa ufumbuzi na nyingine kuahidi kuwasilishwa kwa Mtendaji Mkuu.

Aidha, wataalam waliazimia kwa pamoja kushirikiana na manegimenti ya GST kuhakikisha wanatekeleza adhima hii na wakashauri viwepo vikao vya mara kwa mara vya kiutendaji kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa majukumu na kupeana mrejesho.

Previous articleNAIBU WAZIRI MKUU DOTO BITEKO ATEMBELEA BANDA LA STAMICO MAONESHO YA MADINI GEITA
Next articleGAVANA TUTUBA: DHAHABU YA TANZANIA KUSAJILIWA KWENYE SOKO LA DUNIA LONDON
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here