Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea Banda la Benki hiyo, kujionea shughuli wanazofanya katika maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Bomba mbili – EPZ leo Septemba 23,2023, Mkoani Geita.
(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)
GEITA.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesema kuwa jumla ya kilo 418 za Dhahabu tayari zimeshafirishwa kwenda nchini Uingereza kwaajili ya kuisajili kwenye soko la kimataifa na mfuko wa kuhifadhi dhamana na hifadhi za Kimataifa.
Gavana Tutuba amebainisha hayo leo Septemba 23, 2023 kwenye Mahojiano na waandshi wa habari wakati wa ziara yake fupi ya kutembelea Banda la BoT kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ – Bomba mbili Mkoani Geita.
Amesema kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi ya Tanzania toka ipate Uhuru, Serikali ilikuwa ikitunza fedha za kigeni ikiwemo Dola lakini sasa imeingia kwenye historia ya nchi zinazo hifadhi Dhahabu kutoka Tanzania.
“Tayari kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru tulikuwa tunatunza na kuhifadhi fedha za kigeni ikiwemo Dola, lakini kwa mara ya kwanza sasa imengia kwenye historia ya nchi zinazo hifadhi dhahabu ambayo imenunuliwa Tanzania,”amesema.
Ameeleza kuwa wamejipanga kuendelea kununua Dhahabu kwa wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa, pamoja na wauzaji wengine waliopo kwenye maeneo mbalimbali, na kwamba wanaendelea kuhamasisha wananchi kutembelea banda la BoT kupata elimu na kufahamu namna ambavyo wanaweza wakauza dhahabu yao kupitia Benki hiyo.
“Hivi sasa kwenye Maonesho haya tunaendelea kuhamasisha watu waje kupata elimu na kufahamu namna ambavyo wanaweza wakauza dhahabu yao kupitia BOT.
“Kwasababu sisi tunanunua wenyewe, tunatoa bei halisi ya soko kwa siku hiyo, tofauti na wengine ambao wamekuwa wakinunua kwa bei za chini, inawekana isiwape manufaa makubwa kama wanavyotarajia” ameeleza Gavana Tutuba,
Aidha amesema kuwepo kwao kwenye maonesho hayo kumetoa fursa kwa wananchi kufahamu mifumo yao ya kudhibiti uharifu kutokana na uwepo wa wachimbaji na baadhi ya wadau wa madini kupokea fedha nyingi au kutumia fedha tasilimu katika miamala yao ya kulipa au kupokea fedha hizo.
kutokana na changamoto hizo, BoT imetengeneza Mfumo ya kurahisisha unaoitwa ‘Tanzania Payment System’ (Tips). uliounganishwa mabenki yote na watoa huduma wa miamala kwa njia ya kampuni za simu.
“Kwa kutumia mfumo huu, umepunguza gharama za kuhamisha miamala kutoka Kampuni moja kwenda nyingine au kubadilishana kutoka benki moja kwenda nyingine” amesema Gavana Tutuba.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, (wa pili kushoto) akitoa Maagizo kwa Meneja Msaidizi Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha za kigeni nchini, Dkt. Anna Lyimo (kulia), alipokuwa katika ziara fupi ya kutembelea Banda la Benki hiyo, katika Maonesho hayo. (wa kwanza kushoto), ni Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (wa pili kushoto), akimsikiliza Bw. Ephraim Madembwe, Mchambuzi Mwandamizi Masuala ya fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT). (wa kwanza kushoto), ni Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (wa pili kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi Mkuu katika Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo Bi. Kidee Mshihiri (kulia), alipokuwa akielezea kazi na majukumu yanayotekelezwa na kurugenzi yao. (wa kwanza kushoto), ni Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (katikati) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella (kushoto) wakati Mkuu wa Mkoa huyo alipofika katika Banda la Benki hiyo kukutana na Gavana pamoja na kujionea namna BoT inavyotekeleza Majukumu yake katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ – Bomba mbili Mkoani Geita. (kulia), ni
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, (katikati), akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Emmanuel Tutuba, (kushoto), wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipofanya ziara fupi kwenye Banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya Madini Geita. (kulia), ni Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Martin Shigella, (kushoto), akiagana na Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Victoria Msina, (kulia), mara baada ya kumaliza mazungumzo yake mafupi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (katikati), katika Banda hilo.
Baadhi ya watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), katika picha ya pamoja.
(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)