Home LOCAL WIKI YA AZAKI 2023 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR 

WIKI YA AZAKI 2023 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR 

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga, (wa pili kushoto), akiwa na Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustini Ndugulile pamoja na wadau wengine wakipiga makofi mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi rasmi wa Wiki ya Azaki iliyozinduliwa leo Agosti 1,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Azaki iliyofanyika leo Agosti 1, 2023, Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Wiki ya AZAKi 2023, Justice Rutenge akizungumza katika hafla hiyo kuelezea namna kaulimbiu ya mwaka huu ilivyobeba dhima nzima ya Wiki ya Azaki.

Picha za wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa (FCS), Francis Kiwanga, (wanne kushoto), akiwa na Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile (wa tano kushoto), pamoja na wadau wengine katika picha ya pamoja katika hafla hiyo.

(PICHA ZTE NA: FCS)

 Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga, amesema kuwa Teknolojia yanaweza kuwa chachu ya kuongeza kasi ya maendeleo pamoja na kuwawezesha watanzania kuongeza uzalishaji, kutafuta masoko na hatimaye kukuza vipato vyao.

Kiwanga ameyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa Wiki ya Azaki iliyofanyika leo Agosti 1, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa lengo la kuwepo kwa Wiki ya Azaki ni kutazama kwa jinsi gani maendeleo ya teknolojia yanavyoweza kuwawezesha watanzania kuongeza uzalishaji, kutafuta masoko na hatimaye kukuza vipato vyao.

Aidha ameeleza kuwa mwaka 2018 Wiki ya Azaki ilifanyika kwa mara ya kwanza ambapo pamoja na mambo mengine walijifunza namna ya kuimarisha mahusiano yao na Serikali.

“Mnamo mwaka 2018 tulikutana kwa mara ya kwanza kwa ajili ya CSO Week, tulianza kujiuliza tunawezaje kuimarisha mahusiano yetu na Serikali.

“Lengo jingine lilikuwa ni kuwajengea uwezo (Capacity Building) kwa wananchi wa kawaida, ili kuweza kuboresha maisha yao, na kuleta tija katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo wananzozifanya” ameeleza Kiwanga.

Pia ameongeza kuwa, kufanyika kwa Wiki ya Azaki mwaka huu kutakuwa ni mwendelezo ikiwa ni mara ya tano kuzindua ikiwa ni  kuelekea kwenye Wiki ya Azaki itakayofanyika mwezi Ogasti 2023, lengo likiwa ni kuwagusa wananchi wanaowapa nguvu ya kufanyakazi kila siku.

“Mimi Binafsi kwa mfano, ninapata nguvu ya kufanya kazi kila ninapoona picha ya mama mmoja toka kijijini, akiwa na furaha na tabasamu kubwa baada ya kupata mavuno yake, hawa ndio wanaotupa msukumo wa kuendelea kufanya kazi na kufanya CSO Week kila mwaka” ameongeza Kiwanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wakili Anna Henga, ameweka wazi kuwa moja ya haki za msingi za binadamu ni kufikia huduma za teknolojia ambapo amebainisha kuwa ukuaji wa Sayansi na Teknolojia utawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na haki zao kupitia vifaa vya teknolojia.

Wiki ya Azaki inaleta pamoja Asasi za Kiraia ( AZAKI ) Pamoja kutoka Tanzania nzima kwa ajili ya tukio la wiki moja lenye lengo la kujadili na kuboresha ushirikiano wa kimkakati ikiwa na Kauli mbiu isemayo ‘ Teknologia na Jamii . Tulipotoka, tuilipo sasa na tunapoelekea , kuangazia fursa na changamoto zinazotokana na ulimwengu wa teknolojia unaoendelea’

Mratibu wa Wiki ya AZAKi 2023, Justice Rutenge ameelezea kuhusu uchaguzi wa kaulimbiu ya mwaka huu iliyobeba dhima nzima ya Wiki ya Azaki ambapo amesema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa madhumuni, na inalenga kuziwezesha asasi za kiraia kufahamu na kupata utaalamu unaohitajika ili kuishauri Serikali na Sekta Binafsi juu ya faida na vikwazo vinavyotokana na teknolojia kwa maendeleo ya nchi.

Wiki ya Azaki inatajiwa kuanza rasmi tarehe 23 hadi 27 Oktoba 2023 Jijini Arusha, ambayo inatokana na mafanikio ya matoleo yake ya awali ya mwaka 2018, 2019, 2021 na 2022, ambapo kwa mwaka huu inatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko, kukuza uelewa wa kina wa athari za teknolojia kwa jamii na nafasi yake inayowezekana katika kuunda.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO AGOSTI 1,2023
Next articleMAKAMU WA RAIS AFUNGUA NANENANE 2023 MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here