Home BUSINESS WAZIRI MSTAAFU PINDA ATAKA UDHIBITI WA UZALISHAJI VIFARANGA VYA SAMAKI

WAZIRI MSTAAFU PINDA ATAKA UDHIBITI WA UZALISHAJI VIFARANGA VYA SAMAKI

Wazairi Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ameitaka Serikali kudhibiti uzalishaji holela wa Vifaranga vya Samaki ili kuwasaidia wafugaji kupata mbegu bora ya Vifaranga vya Samaki

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ameyasema hayo mkoani Morogoro kwenye Maonyesho ya wakulima Nanenane Kanda ya Mashriki wakati alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Amesema kuna haja ya kuwepo kwa Mamlaka itakayo kuwa inasimamia ubora wa Vifaranga vya Samaki ili mfugaji anapopata Vifaranga visivyokuwa na ubora kuwe na Sehemu ya Kutoa Taarifa na kupata msaada.

Aidha, Pinda amekipongeza Chuo cha SUA kwa kuwajali wakulima na wafugaji kwa kuja na teknolojia mpya Katika maonesho hayo zitakazowasaidia kuongeza ujuzi na kuzalisha tija.

Awali akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Afisa Mafunzo Shamba la Mafunzo ya Mfano kutoka SUA Bi.Stella Genge amesema SUA kupitia Ndaki ya Kilimo, Idara ya Sayansi ya Wanyama, Viumbe Maji na Malisho imejikita katika kuzalisha vifaranga vya samaki na kutoa elimu bora jinsi ya kutunza samaki, pia inazalisha chakula cha samaki majani aina ya azola ambayo ni mojawapo ya chakula kizuri cha Samaki na Mifugo mingine kama vile kuku, ng’ombe na wanyama wengine wafugwao.

Previous articleTARI IMEJIPANGA KUWANUFAISHA WAKULIMA KWA KUPATA MBEGU BORA, ZENYE TIJA
Next articleRC MTAKA ATEMBELEA BANDA LA EWURA, ASIFU UFANISI WA HUDUMA ZAO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here