Home BUSINESS TARI IMEJIPANGA KUWANUFAISHA WAKULIMA KWA KUPATA MBEGU BORA, ZENYE TIJA

TARI IMEJIPANGA KUWANUFAISHA WAKULIMA KWA KUPATA MBEGU BORA, ZENYE TIJA

Na: Neema Adriano

TARI Ilonga imekuja na Teknolojia mbalimbali ambazo zinazalishwa na kituo Cha Ilonga pamoja na vituo mbalimbali hasa vituo vilivyopo Kanda ya Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti, 4, 2023,katika Viwanja vya Nanenane Morogoro Mratibu wa Kitaifa wa utafiti wa Mtama,Ulezi na Uwele, Bw.Emmanuel Thomas Mwenda amesema wamewaletea wakulima Teknolojia ambayo itawasaidia kupata mavuno yenye tija.

Amesema mazao mengi ambayo wameyaleta katika Viwanja hivyo yanalimwa na wakulima katika maeneo ya Kanda ya Mashariki ikiwemo mazao ya Mtama, Ulezi na Uwele pamoja na mazao mengine mengi.

“Teknolojia kubwa ambazo tumezileta Moja ni mbegu Bora lakini pili ni kanuni bora za kiagronomia ambazo tunamshauri mkulima aweze kuzitumia ili aweze kuzalisha kwa tija.

“Mbegu tulizoleta kwa zao la Ulezi ni tatu ambazo zimetafitiwa na zina tija kubwa,mbegu hizi ni P224, U15 pamoja na TARI FM1, mbegu hizi tatu zina uwezo wa kuzaa kuanzia Tani 2 mpaka Tani 4 kwa hekta moja haya ni mavuno makubwa sana ukilinganisha na mbegu zile za kienyeji ambazo zinatumiwa na wakulima wengi.

Ameendelea kusema kuwa kwa upande wa zao la Mtama, TARI imeleta mbegu aina ya Macia ambayo ni Mtama mweupe, mbegu aina ya TARI SOR2 ambayo pia mi Mtama mweupe, na mbegu aina ya TARI SOR1 ambao yenyewe ina rangi ya kahawia.

“Hizi ni mbegu Bora ambazo zina sifa tofauti tofauti nikianza na mbegu aina ya Macia yenyewe Ina uwezo wa kutoa mavuno kati ya Tani 3.5 mpaka Tani 4 kwa hekta Moja, yaani magunia 35 mpaka 40 kwenye hekta Moja endapo mkulima atatumia kanuni bora za kiagronomia, mbegu hii Ina uwezo wa kuzaa vizuri kuanzia ukanda wa chini mpaka ukanda wa kati na Ina uwezo wa kutoa mavuno hayo niliyoyasema.

Pia Bw.Mwenda amesema Mbagu ya TARI SOR2 yenyewe Ina uwezo wa kuzaa tani 3 mpaka Tani 3.6 kwa hekta moja na mbegu hiyo Ina sifa ya ziada ya kuweza kukabiliana na gugu chawi aina ya kiduha ambayo inasumbua sana katika maeneo ambayo yana upungufu sana wa rutuba au eneo lenye kichanga.

Njia shirikishi ambayo unaweza kuitumia katika kukabiliana na gugu chawi hili mojawapo ni kutumia mbegu zenye ukinzani na gugu hilo ambao ni kama hii niliyoisema.

Ameeleza kuwa njia nyingine ya pili ni pamoja na matumizi ya mbolea hasa samadi lakini pia namna bora ya kufanya kilimo Cha mzunguko lakini njia hii Sasa ya kutumia mbegu ambayo yana ukinzani inaonekana kufanya vizuri zaidi kwa wakulima ambao wana ardhi ndogo ambayo wanaitumia na wanaitegemea ardhi hiyo katika kuzalisha zao hilo Moja tu.

“Mbegu ya tatu ni TARI SOR1 ni mbegu ambayo rangi yake ni kahawia Ina uwezo wa kuzaa tani 3 mpaka Tani 3.6 kwa Hekta Moja,sifa yake nyingine ya ziada ni uwezo wake wa kukabiliana na gugu chawi linalojukikana kama kiduha.

Hivyo amewashauri wakulima wanaokabiliwa na changamoto ya gugu aina ya kiduha katika mashamba Yao kuweza kutumia mbegu za Mtama zenye ukinzani ili waweze kulima kwa tija.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 5 – 2023
Next articleWAZIRI MSTAAFU PINDA ATAKA UDHIBITI WA UZALISHAJI VIFARANGA VYA SAMAKI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here