Home LOCAL WANAFUNZI WAPATIWA ELIMU KUKABILIANA NA AJALI

WANAFUNZI WAPATIWA ELIMU KUKABILIANA NA AJALI

Dereva wa Bajaji jijini Tanga Avishai Fanuel akiandika maelezo ya kotorudia kosa la kutosimama katika kivuko cha waenda kwa miguu baada ya kukamatwa na Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani na kisha kufikishwa katika Mahakama ya Watoto iliyokuwa ikiendshwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwakizaro mkoani Tanga.Katikati anayeshudia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga William Mwamasika.Mahakama ya Watoto ni sehemu ya Mpango wa Shirika la Amend kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kuwajengea uelewa wanafunzi kutambua sheria ili kujieupusha na ajali.

Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akielezea hatua waliyofikia katika kuutekeleza Mpango Kazi wa Usalama Barabarani kwa Jiji la Tanga baada ya kufanyika kwa Mahakama ya Watoto waliokuwa wakisimamia kesi za madereva waliokiuka sheria za usalama barabarani.

Mkufunzi wa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda akitoa ufafanuzi wa michoro mbalimbali ya usalama barabarani kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga ( hayuko pichani).

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga William Mwamasika (katikati) akizungumza baada ya kumalizika kwa uendeshaji kesi za madereva waliokiuka sheria za usalama barabarani uliokuwa ukisimamiwa na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwakizaro jijini Tanga.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwakizaro wakiendesha kesi katika Mahakama ya Watoto ambayo ilikiwa ikisikiliza kesi za madereva waliovunja sheria za usalama kwa kutosimama eneo la kivuko cha waenda kwa miguu.

Na: Mwandishi Wetu, Tanga

WATOTO wametajwa kuwa kundi muhimu katika kuiandaa jamii yenye kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuepusha ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo, baada ya kukamilisha uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto (Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Kalolo amesema Shirika hilo limeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuijengea jamii uwelewa wa sheria za usalama barabarani ambapo pamoja na mambo mengine Amend imetoa mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa waendesha pikipiki 350 katika Jiji la Tanga.

“Tumeanzisha klabu mbili za shule za usalama barabarani katika Shule ya Msingi Usagara na klabu ya usalama wa baiskeli katika Shule ya Sekondari Usagara, yenye watoto 20 katika kila klabu. Tumetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hawa, baada ya kuhitimu kuwa mabalozi na kupokea vyeti.

“Shughuli za vilabu hivi zimejumuisha mafunzo, midahalo ya usalama barabarani, michezo, mijadala ya mezani na kushiriki katika kampeni za vyombo vya habari. Mahakama Kifani ya watoto katika Shule ya Msingi Mwakizaro, mafunzo ya msasa kwa waendesha pikipiki 350 na kufanya jumla ya madereva waliopata mafunzo haya kufikia 950,” amesema.

Mbali na kutoa mafunzo hayo, pia limetoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi, kuanzisha klabu za usalama barabarani na mahakama kifani za watoto, kuandaa makongamano ya wadau wa usalama barabarani na kufanya utafiti kuhusu ajali za barabarani.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Amend Tanzania Simon Kalolo, baada ya kukamilisha uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto (Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Amesema shirika hilo linajishughulisha na usalama barabarani nchini tangu mwaka 2009 kwa ufadhili wa Shirika la Fondation Botnar jijini Tanga.

Kwa mujibu wa meneja huyo, mpango kazi huo wa usalama barabarani wenye lengo la kuboresha safari salama na endelevu kwa jiji la Tanga ulizinduliwa Novemba 11, 2022 na tangu hapo kuna mambo mbalimbali yametekelezwa.

Kalolo amesema Februari mwaka huu wamesambaza vifaa vya kufundishia usalama barabarani kwa maofisa maendeleo ya jamii katika kata 22 kati ya 27 za Jiji la Tanga.

Pia, amesema Juni mwaka huu maofisa maendeleo ya jamii walikuwa wamezungumza kuhusu usalama barabarani katika zaidi ya mikutano au matukio 50 tofauti, na kuelimisha takriban wananchi 6,600.

“Tumeanzisha kikundi cha jumuiya ya vijana kufanya shughuli katika maeneo tunayofanyia shughuli za shule. Hawa ni vijana ambao awali walishiriki katika mipango mbalimbali ya TangaYetu.

Kwa upande wake Mkuuwa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga William Mwamasika, ameema katika mkoa huo kumekuwa na changamoto ya matukio mengi ya ajali za barabarani hususani sinazowahusu wanafunzi kutokana na waendesha vyombo vya moto kutotii sheria za usalama barabarani.

Amesema licha ya Jeshi la Polisi kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha vyombo vya moto wakwemo waendesha bodaboda, bajaji na magari lakini bado chamoto ya ajali imeendelea kuwepo, hivyo alitoa wito kwa jamii kuheshimu na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Mwamasika ameslishukru Shirika la Amend kwa kuja na mpango huo katika Jiji la Tanga kwani umewezesha kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi pamoja na watumiaji wengine wa vyombo vya moto

Previous articleSIMBA SC YAANZA LIGI KWA KISHINDO IKIICHAPA MTWIBWA SUGAR 4-2 MANUNGU
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 18-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here