Home SPORTS SIMBA SC YAANZA LIGI KWA KISHINDO IKIICHAPA MTWIBWA SUGAR 4-2 MANUNGU

SIMBA SC YAANZA LIGI KWA KISHINDO IKIICHAPA MTWIBWA SUGAR 4-2 MANUNGU

Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kunyakua pointi 3 kwa kuichapa timu ya Mtibwa sugar mabao 4 -2 katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Manungu, Morogoro.

Katika mchezo huom timu ya Mtibwa Sugar walikuwa imara kwenye mashambulizi ya kushtukiza pamoja na kujilinda kwa tahadhari huku wakikosa kutumia nafasi ambazo walizipata.

Mabao ya Simba yamefungwa na Jean Baleke dakika ya 5, Willy Onana dakika ya 9, Fabrice Ngoma dakika ya 44 na Clatous Chama dakika ya 80.

Mabao ya Mtibwa sugar yamewekwa kambani na mshambuliaji wake Matheo Anthony katika dakika ya 20 na 22 kipindi cha kwanza na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya 2-2

Previous articleRAIS SAMIA APOKEA MACHAPISHO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 IKULU CHAMWINO DODOMA
Next articleWANAFUNZI WAPATIWA ELIMU KUKABILIANA NA AJALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here