Home LOCAL WAANDISHI WA HABARI KUFANYA ZIARA MKOANI MARA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA...

WAANDISHI WA HABARI KUFANYA ZIARA MKOANI MARA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA PEPFAR

Na:  Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo Mbalimbali vya Habari nchini Tanzania wanatarajia kufanya ziara ya siku tano kuanzia Agosti 14,2023 Mkoani Mara kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI – The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) nchini Tanzania.
Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania ilianzisha Mpango wa PEPFAR mnamo mwaka 2003 baada ya Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush kutangaza Mpango wa Dharura wa Kukabiliana na UKIMWI. 
 
Kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) kupitia Amref Health Africa Tanzania wanatekeleza afua mbalimbali za afya mkoani Mara.
Sehemu ya Waandishi wa Habari kutoka Vyombo Mbalimbali vya Habari nchini Tanzania na wadau wa afya wakiwa katika picha ya pamoja leo Jumamosi Agosti 12,2023 kabla ya kuanza kufanya ziara Mkoani Mara kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania.

Previous articleKIGAHE  AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUWA WAADILIFU KATIKA HUDUMIA ZAO 
Next articleGETHSEMANE – GROUP KINONDONI (GGK) KUJA NA VIDEO YA DUNIA HII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here