Home ENTERTAINMENTS GETHSEMANE – GROUP KINONDONI (GGK) KUJA NA VIDEO YA DUNIA HII

GETHSEMANE – GROUP KINONDONI (GGK) KUJA NA VIDEO YA DUNIA HII

Na: Mwandishi Wetu

KWAYA maarufu nchini ya Gethsemane inayosali Kanisa la wasabato Kinondoni, ipo mbioni kutoa video ya wimbo wake mpya unaofahamika Dunia hii.

Taarifa iliyotolewa leo Agosti 13, 2023 jijini Dar es Salaam na uongozi wa Kwaya hiyo yenye makazi yake Kinondoni imesema video hiyo imegusa uhalisia wa maisha katika Dunia tunayoishi. Video hiyo imefanywa na Director Joowzey.

Pia video ya wimbo huo ambayo itatoka Jumamosi ya wiki hii itakuwa kwenye albam yao ya Bado Kitambo, ambayo nyimbo zake zimeendelea kujizolea umaarufu na kupendwa na wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili.

“Mnaweza kuuliza lengo la wimbo ni nini? Jibu; lengo ni kuwaambia watu kuwa Mungu anatoa faraja kwa watu wote wanaopitia Mapito/ shida mbalimbali na changamoto za dunia.

“Na video ya wimbo huo tunaitumia kama zawadi kwa mashabiki wetu wa nchini Kenya kwani kwaya yetu wiki hii yote na wiki ijayo tupo Kenya tukiendelea kuhudumu kwa Nyimbo Kwenye mikutano ya Injili, (Makambi) “ imesema taarifa hiyo.

Kuhusu Mipango ya Gethsemane imesema pamoja na mambo mengine wanayoendelea kuyafanya wanatarajia kuzindua album yao ya Bado Kitambo mwishoni mwa mwaka 2023.

Previous articleWAANDISHI WA HABARI KUFANYA ZIARA MKOANI MARA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA PEPFAR
Next articleWATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA, WAKUU WA BODI KUKUTANA ARUSHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here