Home LOCAL VIONGOZI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA CHUO KIKUU MZUMBE

VIONGOZI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA CHUO KIKUU MZUMBE

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Masoko wa Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Ester Kiondo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Jijini Mbeya. 

Akiwa katika banda hilo Mhe. Hussein Bashe ameahidi kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mbili na laki tano kwa Mercy Mwambe, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya usimamizi wa biashara katika ujasiriamali na ubunifu kwa ajili ya kununua mashine ya kutengenezea mafuta ya kupaka yanatokana na zao la Mchikichi. 

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Jijini Mbeya.

Waziri wa Kilimo Mh. Hussein  Bashe akipata maelezo wakati alipokuwa katika banda hilo. 

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza na Dk. Aloyce Gervas, Mwakilishi wa Kurugenzi ya ukimataifaji na Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipokuwa akimshukuru kwa kutembelea Banda la Chuo Kikuu Mzumbe.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh. Anthony Mtaka akipokea zawadi wakati alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Mzumbe kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. 

Previous articleBRELA, LGAs ZATAKIWA KURAHISISHA UTOAJI LESENI
Next articleRC MTAKA ATEMBELEA BANDA LA TCAA, ASIFU UFANISI WA TAASISI HIYO MAONESHO YA NANENANE MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here