Home BUSINESS VETA KUPANUA MAFUNZO YA UFUNDI SIMU NCHINI

VETA KUPANUA MAFUNZO YA UFUNDI SIMU NCHINI

Meneja Uhusiano wa  Mamlaka ya Ufundi Stadi VET  Bw. Sitta Peter  akizungumza kuhusu namna watakavyopanua mafunzo ya ufundi simu katika vvyuo vingine katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

 Mnufaika na elimu ya mafunzo ya ufunfdi simu  ambae amehitimu katika chuo Cha VETA Kipawa Unice Kavishe akitoa maelezo kwa wananchi waliopita  katika banda lake  lililopo banda kuu ya VETA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Mnufaika na elimu ya mafunzo ya ufunfdi simu  ambae amehitimu katika chuo Cha VETA Kipawa Unice Kavishe akitoa maelezo kwa wananchi waliopita  katika banda lake  lililopo banda kuu ya VETA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

  Mnufaika na elimu ya mafunzo ya ufunfdi simu  ambae amehitimu katika chuo Cha VETA Kipawa Unice Kavishe akifafanua jambo na kuonesha baadhi ya vitendea kazi vyake wakati akitoa maelezo kwa wananchi waliopita katika banda lake lililopo banda kuu ya VETA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Mamlaka ya Ufundi Stadi VETA inatarajia kupanua elimu ya mafunzo ya ufundi simu nchi nzima ili kusaidia taaluma hiyo kutoa ajira Kwa vijana wengi nchini

Akizungumza jijini Mbeya kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Meneja Uhusiano wa mamlaka hiyo Bw. Sitta Peter amesema wazo la mafunzo ya ufundi simu za mkononi lilianza na chuo Cha Tehama VETA Kipawa likiwa kama mradi ambao unapata msaada kutoka kwenye mradi wa SDF na mamlaka ya mawasiliano TCRA.

Amesema VETA Kipawa iliweza kufundisha vijana wengi na kuratibu mafunzo kwenye maeneo mengine ikiwemo Dodoma, Mbeya,Kigoma na Arusha kwa sababu huko tayari kulikuwa na miundombinu ya mafunzo ya Tehama.

Kwa kuangalia uhitaji wa maombi mengi sana kuna wakati yanafika mpaka 200 watu wameomba na pengine nafasi zilizopo ni 100 TU Kwa hiyo tukaona uhitaji ni mkubwa hivyo kwa  sasa  tunaangalia uwezekano wa kupanua mafunzo yasiendelee TU kuratibiwa na VETA kipawa Bali yatolewe Moja Kwa moja kwenye vyuo bila kuwa na mradi”amesema Bw.Peter

Aidha Peter ameongeza kuwa  mafunzo hayo yataanza kwenye vyuo vya VETA ambavyo vinatoa mafunzo ya elekroniki ambapo kwenye vyuo hivyo Kuna vifaa ambavyo ni rahisi kutoa mafunzo ya simu za mkononi.

“Mpaka Sasa vyuo vinavyotoa mafunzo ya elekroniki ni VETA Dodoma,VETA Kigoma lakini pia tunawaza kufanya hivyo kwa vyuo vya Veta  Mbeya na Arusha na mipango ipo kwenye hatua za awali lakini Lengo letu ni kupanua elimu hii ili vijana waweze kujiajili”ameongeza Peter.

Kwa upande wake mnufaika na elimu hiyo Unice Kavishe ambae amehitimu katika chuo Cha VETA Kipawa na kujiajili katika soko la kariakoo jijini Dar es salaam na kuwa mbobezi katika eneo hilo Ameishukuru Veta na akieleza kuwa Veta ni kama vile Baba  mlezi wa familia kwani imemtoa mbali na kumfungulia duni katika maisha yake.

Amesema kazi hiyo inamsaidia kuongeza kupata kipato cha kutosha tu na kuendesha  familia yake huku akipanua biashara yake kwa kuanzisha karakana yake mwenyewe eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam jambo linalmfanya ajiamini katika maisha.

Unice Kavishe ameongeza kuwa  fani ya ufundi simu imekua ya tofauti na fani nyingine Kwani inatengeneza mazingira ya kujiajili mwenyewe na si kusubiri ajira huku kadri unavyofanya kazi ndio unavyozidi kupata uzoefu kubobea kwenye kazi hiyo.

“Nawasihi sana hasa wakina dada kukaa nyumbani na kupoteza muda bila kufanya kitu chochote wakati kunakazi nyingi za kufanya itawafanya kuwaza mambo yasiyo ya msingi katika maisha yao Kwani ukiifanya hii kazi Kwa uaminifu inakutengenezea kipato kikubwa sana”amesema Kavishe,

Aidha Kavishe ameipongeza serikali kwa kuona kozi hiyo inawafaa vijana wengi na lakini ada zake zimekuwa rafikiambapo mtu wa kipato chochote anaweza kusomea na ni ya muda mfupi.

“Watu wengi wanaipenda kazi hii kupitia Mimi na wanajifunza kupitia kuniona Sasa nimekua dira Kuna watu walikua hawajui fani inapatikana wapi lakini nimewasaidi na wengi wamesoma na Wana vyeti vyao na tayari wameanza kujiajili hivyo Sasa miundombinu inahitajika Kwani uhitaji ni mkubwa “ameongeza Kavishe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here