Home SPORTS TIMU YA TANZANIA PRISONS IPO IMARA KUANZA LIGI KUU MSIMU MPYA

TIMU YA TANZANIA PRISONS IPO IMARA KUANZA LIGI KUU MSIMU MPYA

Na: mwandishi wetu
UONGOZI  wa timu ya Tanzania Prison umeweka wazi kuwa umejipanga vyema kuhakikisha wanafanya vyema katika msimu ya wa ligi kuu 2023/2024.
Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa jezi zao, Kamishina Jenerali wa Mageraza Mzee Ramadhan Nyamka amesema kuwa Prisons ni miongoni mwa timu kongwe  katika Ligi kuu hivyo wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi wamejipanga kuhakikisha wanafanya vyema msimu huu.
“Timu hii ni miongoni mwa timu kubwa hapa Tanzania hivyo tumejipanga kuhakikisha wachezaji pamoja na viongozi wanafanya vyema katika kuhakiksha timu inapata matokeo mazuri ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya kitaifa”amesema
Ameongeza kuwa msimu huu ni msimu wa Tanzania Prisons kwa kufanya vyema katika ligi kutokana na maandalizi ambayo wamejiandaa pamoja na wachezaji ambao wamewasajili.
“Nitashirikiana na wachezaji  pamoja na viongozi bega kwa bega  kuhakikisha timu inafanya vyema katika ligi kwa kupata matokeo mazuri”
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Wakazi Kelvin Ndawi amesema kuwa anajivunia kutengeneza jezi nzuri za Tanzania Prison kwa msimu huu.
Ameongeza kuwa ameingia mkataba wa mwaka mmoja katika utengenezaji wa jezi pamoja na vifaa vya michezo vya timu hiyo.
“Najivunia kutengeneza jezi nzuri kuliko timu zote zinazoshiriki ligi kuu hivyo basi nina imani kikosi kitafanya vyema msimu huu” amesema.
Previous articleWATOTO WAWILI WAUAWA KWA KUNYONGWA, BABA YAO AKUTWA AMEJIUA JUU YA MTI
Next articleRAIS DKT. SAMIA AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA MCHANGO WAKE KATIKA. KILIMO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here