Home LOCAL TCU YATOA TAARIFA MWENENDO WA UDAHILI MWAKA WA MASOMO 2023/203

TCU YATOA TAARIFA MWENENDO WA UDAHILI MWAKA WA MASOMO 2023/203

  Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) katika mkutano wake uliofanyika kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2021. 

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa mwenendo wa Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/2024, ambapo zoezi la kuthibitisha Udahili kwa waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi yakimoja katika awamu ya kwanza Udahili litakamilika rasmi Septemba 6, mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuelezea mwenendo mzima wa udahili kwa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza kwa Mwaka wa masomo 2023/2024, katika Ofisi za Tume hiyo leo Agosti 29,2024 Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa, zoezi hilo linakwenda vizuri, na kwamba mara litakapokamilika, zoezi litakaloendelea ni Vyuo kuchakata na kuidhinisha maombi ya udahili yaliyopelekwavyuoni katika Awamu ya pili ya Udahili.

“Zoezi la kuchakata na kuidhinisha maombi hayo litakapokamilika, majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Pili ya Udahili yatatangazwa na vyuo husika Septema 20, mwaka huu” amesema Prof. Kihampa.

Aidha Prof. Kihampa ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa Awamu ya Pili ya Udahili, Awamu ya Tatu ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/2024 itaanza rasmitarehe 25 hadi 29, 2023, na kwamba Tume hiyo inawasisistiza waombaji ambao bado hawajatuma maombi yaudahili mpaka sasa, watumie muda huo uluobakivizuri kutuma kwa usahihimaombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipendaa.

“Tume inaelekeza Taasisi za Elimu ya Juu nchini, kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafas. Aidha waombaji wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kama inavyoonekana kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU ya (www.tcu.gotz)” ameeleza Prof. Kihampa. 

Akizungumzia mwenendo wa Udahili, amesema kuwa mpaka sasa jumla ya waombaji 23,387 waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja kati ya43,213 wamejithibitisha katika chuo kimojawapo, na kuwasisitiza wale ambao bado hawajajithibitisha wahakikishe uthibitisho wao kwa kupitia akaunti zao kwenye vyuo wanavyovipenda.

“Naomba kuwahakikishia waombaji wote kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa Chuo kwa kushindwa kujithibitisha” amesisitiza Prof. Kihampa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here