Home LOCAL TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA PILI, YAWAASA WAOMBAJI KUEPUKA UPOTOSHAJI

TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA PILI, YAWAASA WAOMBAJI KUEPUKA UPOTOSHAJI

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) katika mkutano wake uliofanyika kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 23,2021. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, AR ES SALAAM

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa Awamu ya pili ya udahili wa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kuanzia Agosti 25 hadi Septemba 6, Mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Agosti 25,2023 kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa wa TCU Profesa Charles Kihampa, amesema kuwa Dirisha hilo limefunguliwa ili kuendelea kutoa nafasi kwa wananfunzi wenye sifa ya kujiunga na Elimu ya Juu, ambapo ameendelea kusisitiza  kuwa, waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali wanaweza kuitumia  fursa hiyo kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

Aidha Profesa Kihampa amezielekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu chini, kutangaza Programu ambazo bado zina nafasi.

“Waombaji Udahili na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa Udahili wa Awamu ya pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya Udahili iliyoko kwenye tovuti ya TCU ya www.tcu.go”. ameelekeza Prof. Kihampa.

Aidha amewakumbusha waombaji wote wa udahili wa Shahada ya kwanza kuwa masuala yote yanayohusiana na udahili au kujithibitisha kwenye Chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

“kwa wale waombaji ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa” Ameongeza Prof. Kihampa.

Pia amesema, TCU inawaasa wananchi wote kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri na kudai kutoa huduma ya kusaidia jinsi ya kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini. 

Awali akitoa taafa ya udahili wa Awamu ya kwanza,  Prof. Kihampa, amesema jumla ya waombaji 86,624 sawa na asilimia 74.6 ya waombaji wote walioomba udahili wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba, na kwamba mwenendo wa udahili wa Awamu ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia (2019/2020 hadi 2023/2024), kunaonesha ongezeko la waombaji wenye sifa ya kidato cha Sita na wale wa Stashahada.

Idadi ya waliodahiliwa katika Awamu ya Kwanza ya Udahili kwa kipindi cha miaka mitano (2019/2020 hadi 2023/2024), nayo imekuwa ikiongezeka” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here