Home LOCAL MATUMIZI YA TEKNOLOJIA MBADALA YAPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZJI WA BARABARA KWa ASILIMIA...

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA MBADALA YAPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZJI WA BARABARA KWa ASILIMIA 50

Dodoma
Matumizi ya Teknolojia mbadala na malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja imeweza kupunguza gharama zaidi ya 50%.

Hayo yameelezwa Jana na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Maelezo jijini Dodoma.

“TARURA imeweka kipaumbele cha kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.

Mhandisi Seff amesema hadi kufikia mwezi Machi,2023 TARURA imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua.

Ametaja mikoa iliyojengwa madaraja hayo ni Kigoma (92),Singida (24), Tabora (5), Kilimanjaro (10), Mbeya(2),Arusha (6), Morogoro (2), Rukwa(3), Pwani (1), Ruvuma (3) pamoja na Iringa (15).

Aidha, amesema bado wanaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.

“Teknolojia hizo ni pamoja na Ecoroads, Ecozyme na GeoPolymer ambao hadi Sasa kwa kutumia teknolojia ya Ecoroads katika jiji la Dodoma imejengwa Kilomita moja(1) ambayo imekamilika na katika Wilaya ya Mufindi zitajengwa Kilomita kumi(10)”Aliongeza

Previous articleTCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA PILI, YAWAASA WAOMBAJI KUEPUKA UPOTOSHAJI
Next articleMWONGOZO WA UANDAAJI NA UANDISHI WA SERA ZA KISEKTA, ZANZIBAR – 2022 WAZINDULIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here