Home BUSINESS TCAA: NI MUHIMU WAKULIMA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA NDEGE NYUKI KUONGEZA UZALISHAJI

TCAA: NI MUHIMU WAKULIMA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA NDEGE NYUKI KUONGEZA UZALISHAJI

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania (TCAA) Yesaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Taasisi hiyo, kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini leo Agosti 2, 2023.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania (TCAA) Yesaya Mwakifulefule, akionesha picha ya ndege nyuki (Drones) na kutoa rai kwa kuwataka wakulima kutumia teknolijia hiyo katika kutekeleza majukumu yao likiwemo la umwagiliaji na unyunyiziaji wa Dawa kwenye Mashamba yao.

Mbeya Meneja Masoko na Mawasiliano wa (TCAA) Yesaya Mwakifulefule akizungumza na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa mfuko wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi (kulia), wakati alipotembelea Banda la Mamlaka hiyo, kwenye Maonesho Nanenane Jijini Mbeya.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza na Enock Bwigane Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, MBEYA.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wadau wa sekta ya kilimo kutembelea Banda lao katika maonesho ya wakulima nanenane kwa ajili ya kujifunza teknolojia mpya ya ndege nyuki (Drone) ambayo inatumika katika shughuli mbalimbali za kilimo ikiwemo kumwangilia Dawa pamoja na kupanda mbegu.

Akizungumza leo tarehe 2/8/2023 katika Maonesho ya Wakulima Nanenane kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw. Yessaya Mwakifulefule, amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kuhusu matumizi bora ya Ndege Nyuki (Drone), katika shughuli za kilimo ili kuleta tija na kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

“Ni muhimu kutoa elimu kwa wakulimu kuhusu matumizi ya drone ili wajue namna ya kutumia pamoja na kufata taratibu ambazo zimewekwa na TCAA” amesema Bw. Mwakifulefule.

Amesema kuwa ili uweze kutumia drone unapaswa kuomba kibali kutoka TCAA pamoja na kupewa mafunzo ya wiki nne katika Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) ili kujua namna bora ya kuendesha Drone.

*Kuna anga ya chini ambayo unaweza kutumia drone, kati na juu, hivyo tunaendelea kusimamia ili kuepukana madhara yanayoweza kujitokeza katika anga” amesema Bw. Mwakifulefule

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here