Home BUSINESS TASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE MBEYA

TASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE MBEYA

Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania,TASAC Bi. Martha Calvin akizungumza na wananchi mbalimbali hawapo pichani waliotembelea katika  banda la TASAC kwenye maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Johm Mwakangale jijini Mbeya.

(PICHA NA HUGHES DUGILO) 

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania,TASAC ni kati ya Taasisi za Kiserikali zinazoshiriki Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima yanayotambulika kama NaneNane.

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Mbeya yameanza tarehe 1 Agosti na kilele chake ni tarehe 8 Agosti, 2023.Kauli mbiu ya maonesho hayo ni:- “Tanzania: Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo ya Chakula na Usalama wa Chakula ”.

TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanayotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.

TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea banda la TASAC lipo katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.

Previous articleNAIBU WAZIRI MWAKIBETE AIPONGEZA TCAA KWA KUNGANISHA TEKNOLOJIA YA ANGA NA KILIMO
Next articleTCAA: NI MUHIMU WAKULIMA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA NDEGE NYUKI KUONGEZA UZALISHAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here