Afisa Uhusiano Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Renatus Sona akizungumza katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
(PICHA NA : HUGHES DUGUILO)
Na: Hughes dugilo, MBEYA
Wakala wa majengo Tanzania (TBA) imeweka Kambi kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya kutoa elimu kwa wananchi juu ya miradi mbalimbali wanayoisimamia na kutambua shughuli zinazofanywa na wakala huyo.
Afisa Uhusiano wa TBA Renatus Sona amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Viwanjani hapo, na kusema kuwa wamekuwa wakishiriki katika ujenzi wa miliki za serikali ikiwemo ujenzi wa Majengo ya Serikali na nyumba za Makazi nchi nzima.
Aidha ameongeza kuwa TBA imekuwa na miradi mbalimbali ya mkakati Inayoendelezwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo mji wa kiserikali Mtumba mkoani Dodoma ambapo TBA wamekuwa washauri elekezi kwenye mradi huo
Amesema katika mradi huo wa mji wa serikali TBA ni washauri elekezi wanasimamia lakini wanajenga wizara Moja jengo la Wizara ya Ofisi ya Rais Utawala Bora na utumishi wa umma.
Mbunifu Majengo wa Wakala wa Majengo TBAÂ Cecilia Ndumbaro akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la TBA ili kupata ufahamu wa shughuli za taasisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Pendo Palyani Afisa Mawasiliano TBA akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika banda la TBA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.