Home BUSINESS TBA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA NANENANE MBEYA

TBA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA NANENANE MBEYA

Afisa Uhusiano Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Renatus Sona akizungumza katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
(PICHA NA : HUGHES DUGUILO)
Na: Hughes dugilo, MBEYA
Wakala wa majengo Tanzania (TBA) imeweka Kambi kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya kutoa elimu kwa wananchi juu ya miradi mbalimbali wanayoisimamia na kutambua shughuli zinazofanywa na wakala huyo.

Afisa Uhusiano wa TBA Renatus Sona amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Viwanjani hapo, na kusema kuwa  wamekuwa wakishiriki katika ujenzi wa miliki za serikali ikiwemo ujenzi wa Majengo ya Serikali na nyumba za Makazi nchi nzima.

Aidha ameongeza kuwa TBA imekuwa na miradi mbalimbali ya mkakati Inayoendelezwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo mji wa kiserikali Mtumba mkoani Dodoma ambapo TBA wamekuwa washauri elekezi kwenye mradi huo

Amesema katika mradi huo wa mji wa serikali TBA ni washauri elekezi wanasimamia lakini wanajenga wizara Moja jengo la  Wizara ya Ofisi ya Rais Utawala Bora na utumishi wa umma.

Haruna Kalunga Mhandisi Majengo TBA akiwasimamia watoto wakati wakijaza majina yao katika kitabu cha wageni walipotembelea banda la TBA katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Mbunifu Majengo wa Wakala wa Majengo TBA  Cecilia Ndumbaro akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la TBA ili kupata ufahamu wa shughuli za taasisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Msanifu Majengo wa TBA Mtonyi  Chilala  akitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Pendo Palyani Afisa Mawasiliano TBA akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika banda la TBA kwenye  maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Previous articleTASAC YAZIDI KUJIIMARISHA KUWAPA ELIMU WANANCHI MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA
Next articleMKURUGENZI MTENDAJI LATRA ATEMBELEA BANDA LA TCAA MAONESHO YA NANENANE MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here