Mkaguzi wa Vyombo vya Usafiri wa Majini wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kapten Philbert (wa pili kulia), akimsikiliza moja ya Mwananchi aliyetembelea Banda la Taasisi hiyo, katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Iijini Mbeya.
TASAC imepiga Kambi katika maonesho hayo yaliyofanyika kwa wiki moja na yaliyofunguliwa rasmi Agosti 1.2023, na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, ambapo yanatarajiwa kufungwa rasmi leo Agosti 8,2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika Maonesho hayo, wananchi mbalimbali walipata fursa ya kutembelea, na kupita katika Banda la TASAC kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo usalama katika vyombo vya maji, na jinsi Taasisi hiyo inavyotekeleza Majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
Aidha katika Maonesho hayo, TASAC imewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kwa njia ya Maji, kuzingatia sheria na kanuni ili usafiri huo uendelee kuleta tija katika kusafirisha abiria na mizigo.
TASAC ina wajibu wa kusimamia sheria na taratibu zilizopo kwa njia ya Maji, ili kuhakikisha usalama wa vyombo hivyo unakuwepo wakati wote, na kwamba jambo muhimu kwa wamiliki na watumiaji wa vyombo hivyo, kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni zilizopo, ili viendelee kufanya shughuli zake kwa usalama