Home BUSINESS RC MTAKA ATEMBELEA BANDA LA BRELA

RC MTAKA ATEMBELEA BANDA LA BRELA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka, (wa pili kushoto), akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea  Banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakati wa ziara yake ya kutembelea Mabanda ya washiriki, katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale  Jijini Mbeya, leo Agosti 4,2023.

Kiongozi huyo, ametembelea Banda la BRELA kujionea shughuli wanazofanya na kuitaka BRELA kuongeza jitihada katika kuhamasisha wadau kurasimisha Biashara zao ili kukuza uchumi wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka (kushoto),  akipata maelezo kuhusu wageni wanaotembelea Banda la BRELA kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano BRELA, Bi. Rhoida Andusamile (wa pili kushoto) alipofanya ziara katika Banda la Wakala huyo, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane, Agosti 4, 2023 Jijini Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa BRELA katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here