Home LOCAL MKURUGENZI MANISPAA TABORA ELIAS KAYANDABILA ACHAGULIWA KATIBU WA ALAT MKOA WA...

MKURUGENZI MANISPAA TABORA ELIAS KAYANDABILA ACHAGULIWA KATIBU WA ALAT MKOA WA TABORA

Na: Mwandishi Wetu, Tabora

MKURUGENZI wa Manispaa ya Tabora Elias Mahwago Kayandabila amechaguliwa kuwa Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Tabora.

Amechaguliwa katika nafasi ya Katibu wa Jumuiya hiyo kwenye kikao cha ALAT Mkoa wa Tabora kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Aidha wajumbe wa kikao hicho kwa pamoja kabla ya kikao walitembelea miradi mitatu ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo na kuridhishwa na hatua za utekelezaji.

Miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa shule mpya ya Mkoa (Tabora Girls Grand School wenye thamani ya Sh.bilioni 3), ujenzi wa zahanati kwa ufadhili wa TFS na ujenzi wa maduka stendi kuu ya
Kaliua.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya shule ya wasichana mkoani Tabora.

Previous articleMANISPAA YA TABORA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA E-MIKUTANO KUWEZESHA WAJUMBE WALIOKO MBALI KUSHIRIKI
Next articleRAIS SAMIA AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU IDARA YA USALAMA WA TAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here