Home LOCAL KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UWEZESHAJI VIJANA NA WATU WENYE...

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UWEZESHAJI VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 15 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Mendeleo ya Jamii Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 15 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo Bi. Rehema Kipera.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu akionyesha tangazo la mafunzo ya Uanagenzi kwa mwaka wa fedha 2023-2024 kuashiria utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia wasilisho la Utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi wakati wa kikao hicho.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Riziki Lulida akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia), Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (kushoto) wakifuatilia hoja ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao hicho leo tarehe 15 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi wakati wa kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 15 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma.(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU).

Na: Mwandishi Wetu – DODOMA

Kamati ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii imempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ustawi wa vijana na Watu wenye Ulemavu kujikwamua  kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 15, 2023 bungeni na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq kwenye kikao cha kamati cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Aidha, Mhe. Fatuma Toufiq amesema kamati hiyo itaendelea kuishauri Serikali kuendelea kuongeza wigo wa kuwezesha vijana wengi zaidi kupata mikopo, fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa Ofisi yake imefanya maboresho ya mwongozo wa mfuko huo mwaka 2023 ili kupanua wigo wa viwango vya mkopo inayotolewa sambamba na kumwezesha mtu moja moja kukopa badala ya kikundi.

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu amesema kuwa, ofisi hiyo imetenga Sh.Bilioni moja katika mfuko wa Watu wenye Ulemavu kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali za kundi hilo.

Previous articleSERIKALI YAPONGEZA MGODI WA BARRICK BULYANHULU KUENDESHA SHUGHULI ZAKE KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 16, 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here