Home BUSINESS WIZARA YA MALIASILI YAJA KIDIGITALI SABA SABA

WIZARA YA MALIASILI YAJA KIDIGITALI SABA SABA

Wizara ya Malisili na Utalii imeamua kwenda na kasi ya mabadiliko ya sayansi na Teknolojia kwa kuanza kutangaza Utalii kidigitali katika Maonesho ya 47 Kibiashara ya Kimataifa Dar es Salaam, maarufu kama Saba Saba.

Akizungumza baada ya kutembelea banda la Wizara hiyo, Mkurugenzi wa Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Thereza Mugobi amesema, hauwezi kuongelea Utalii bila kuongelea mambo ya kidigitali na ndo maana Wizara imeamua kwenda na mabadiliko hayo ya teknolojia yaliyopo duniani Kwa Taasisi na Idara za Wizara hiyo Kutumia njia ya Kidijitali kuonesha Shughuli na huduma zao mbalimbali.

“Kwenye mabanda yetu watanzania wataweza kuona Utalii wetu kwa kupitia simu janja zao za mikononi (smartphone). Tuna QR Code kwenye kila banda ambazo watanzania wataskani kwa ajili ya kupata vivutio vilivyopo Tanzania nzima na kujua vivutio hivyo pamoja na huduma zinazotolewa na Taasisi zetu” Amesema Dkt. Mugobi.

Amesema katika Maonesho hayo, Wizara imejipanga vyema kuwahudumia wote wanaofika katika banda hilo kwa kasi zaidi kupitia njia hiyo ya kisasa tofauti na ilivyokuwa huko nyuma Taarifa nyingi zilikuwa zikitolewa kwenye vipeperushi ambavyo ni mzigo kwa wageni. 

Aidha Dkt. Mugobi ametoa wito Kwa wananchi kujitokeza Kwa wingi kujipatia huduma mbalimbali kwenye Banda la Maliasili na Utalii ambazo ni njia sahihi na rahisi ya kujipatia fursa mbalimbali kwenye sekta zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Naye Bw. Luca Hakili wa Jijini Dar es Salaam licha ya kupendezwa na huduma inayotolewa na Taasisi mbalimbali za Wizara za Maliasili na Utalii, ameipongeza kwa ufanisi wa taasisi hizo katika kutangaza maliasili zilizopo Tanzania Kisasa zaidi. 

Bw. Hakili ameongeza kuwa kwake imekuwa ni fursa muhimu ya kujua rasilimali lukuki zilizopo nchini nchini na fursa zilizopo kwenye Utalii, Misitu, Wanyamapori pamoja, Malikale na Taasisi zingine.

Pamoja na Mambo mengine, katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii wakazi wa Dar es Salaam wamepata fursa ya kuangalia Filamu ya “Tanzania Royal Tour” iliyosimamiwa na Mhe. Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza baada ya kuangalia filamu hiyo Mtoto, Feisal Seif amefurahishwa kupata fursa ya kuangalia filamu hiyo na kuwataka watoto wenzake kuja kuangalia na kujifunza mambo mengi kuhusu Utalii, uhifadhi, maliasili na kuja kuona wanyapori.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here