Home LOCAL WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA CANADA AWASILI NCHINI

WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA CANADA AWASILI NCHINI

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 19 – 23 Julai, 2023.

   

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Sajjan alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.

Akiwa nchini, Mhe. Sajjan pamoja na ujumbe wake anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali na kujadiliana nao masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Canada.

Aidha, Waziri Sajjan anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Afya pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Canada.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here