Mkurugenzi Mkuu wa Shirikala Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga (wa pilikushoto) akikagua huduma ya Mikutano kwa njia ya mtandao (Video Conference) inayotolewa na Shirika hilo alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Pete Kisenge (wa pilikushoto), akipata maelezo juu ya mfumo unaotumia Kadi maalum ya malipo inayotumika viwanjani (N-Card) kutoka kwa Mtaalamu wa mtandao na usalama wa mtandao Bw. Buchoke Julius, wakati wa ziara fupi ya Mkurugenzi huyo alipotembelea Banda la Shirika hilo kwenye Maonesho ya sabasaba Julai 2,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dk. Peter Kisenge, akipata maelezo kutka kwa Afisa Mwandamizi wa Huduma kwa wateja wakubwa (TTCL) Mary Temba, wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Janet Maeda (kushoto), akiwa na Ofisa Mawasiliano kutoka TTCL Bi Esther Mbanguka (kulia) wakifurahia jambo katika katika banada lao.
(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)
Na: Mwandishi wetu, Dar-es-Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pete Kisenge, amelipongeza Shirika la Mawasiliano nchini, TTCL kwa uwekezaji mkubwa waliofanya kwenye maeneo mbalimbali ikiwepo huduma za Intaneti zitakazowezesha kuimarika zaidi kwa huduma zitolewazo kwenye Taasisi anayoiongoza.
Dkt. kisenge ameyasema hayo Julai 2,2023 alipotembelea Banda la Shirika hilo kujionea kazi na huduma mbalimbali wanazozitoa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita ya Dkt. samia Suluhu Hassan, imefanya uwekezaji mkubwa wa mitambo kwenye Taasisi ya Moyo ya JKCI pamoja na Hospitali nyingine ikiwemo ya Benjamin Mkapa, ambapo kwa kutumia Intaneti za TTCL itawawezesha kuwafikia wagonjwa wengi hasa wale walioko nje ya nchi.
“Kama mnavyofahamu Taasisi yetu ya moyo imezidi kupata wagonjwa wa moyo kutoka nchi mbalimbali hususani Malawi, Commoro, Zimbwabwe, Mozambique na nchi nyingine zaidi ya 20 ambazo wagonjwa wanakuja kupata huduma. Sasa kwa kutumia huduma hii itawapunguzia gharama ya kuja mara kwa mara kukutana na Madaktari wetu pale JKCI.
“Hivyo kwa kutumia Internet hii yenye spidi kubwa sana, kwa kushirikiana na wenzetu TTCL, tunaweza kufanya kitu kinachoitwa ‘Tele Consultation’, yaani, mgonjwa yupo nchi nyingine kama Malawi anaonana na Daktari moja kwa moja aliyepo pale Jakaya Kikwete” ameeleza Dkt. Kisenge.
Amesema kuwa TTCL wana uwezo mkubwa wa kuhifadhi Data mbalimbali na kwamba, itawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa kutokana na uwepo wa mitambo ya MRI, na TC scan, inayotoa picha zenye ujazo mkubwa, hivyo kuhitaji huduma kama hiyo kutoka TTCL.