Home Uncategorized TCAA YAANZISHA MFUKO KUWEZESHA MAFUNZO YA MARUBANI NCHINI

TCAA YAANZISHA MFUKO KUWEZESHA MAFUNZO YA MARUBANI NCHINI

Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)  Hamza Johari, akizungumzana waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Neema Adriano, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya usafiri wa Anga nchini (TCAA) imeanzisha mfuko wa mafunzo ya marubani ili kukabiliana na changamoto ya marubani ambao ni wachache kwa sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Mkurugenzi wa Mamlaka ya usafiri wa Anga (TCAA) Hamza Johari amesema kuwa uhaba wa wataalamu katika sekta ya anga ni mkubwa kwa sababu waliopo hawatoshi ambapo utakuta makampuni ya ndege yaliyopo wananyang’anyana.

“Tunasomesha marubani sasa hivi tumepeleka vijana 10, huko Solati ambao wanasomea masomo ya urubani na wahandisi wa ndege ili walikimaliza waje waajiriwe ili kupunguza changamoto ya marubani.

“Ndio maana siku hizi tumeanzisha Club za wanafunzi kwenye mashule ya sekondari Nchini ili tuende kule kwenye mashule ya sekondari tukachagize ili waweze kupenda masomo ya sayansi kule kwenye masomo hayo ni lazima uwe umefaulu masomo ya Sayansi.

“Na baada ya ufauli mzuri wa digrii Yako basi tutakutangaza kwenye magazeti Nchi nzima na tutakusomesha na mara ya kumaliza masomo Yako utaajiriwa ili kutatua changamoto iliyopo,”amesema.

Kuhusu ubora wa ndege amesema Mamlaka hiyo ndio yenye kupima ubora wa ndege yoyote kabla haijaingia Nchini,ili kujua ubora kabla ya kuruhusiwa kuingia na kuruhusu kufanya kazi na pia ni mdhibiti ambaye anasimamia na kudhibiti sekta ya Anga hapa nchini.

Previous articleRAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JULAI 6 -2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here