Home BUSINESS SUA KUENDELEA KUJIKITA KATIKA TAFITI ZENYE MATOKEO CHANYA KWA TAIFA

SUA KUENDELEA KUJIKITA KATIKA TAFITI ZENYE MATOKEO CHANYA KWA TAIFA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), (kushoto), akishika Tunda aina ya chungwa yanayozalishawa katika SUA ikiwa ni sehemu ya Programu zinazofanywa na chuo hicho. (kulia), ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda  amesema kuwa Chuo hicho kimeendelea kujiimarisha katika shuguli zake za Kitaaluma kwa kutoa elimu yenye ubora sambamba na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi katika kuchochea maendeleo ya Taifa na Jamii kwa ujumla.

Profesa Chibunda ameyasema hayo Julai 18, 2023, alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu namna Chuo hicho kinavyotekeleza majukumu yake, kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) aliyetembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa tafiti zinazofanywa na wanataaluma wa Chuo hicho, zimekuwa na matokeo chanya na kwamba, zimeendelea kuifanya SUA kuwa kinara katika utoaji wa elimu bora inayowawezesha vijana wa Kitanzania kujiajiri wenyewe mara wanapohitimu masomo yao.

“Serikali kupitia Chuo imekuwa ikitoa fedha kwa wataalamu kwa ajili ya kufanya tafiti ili kupata suruhisho la changamoto  zinazoikumba nchi hasa katika  masula mbalimbali ikiwemo kilimo” ameeleza Profesa Chubunda.

Naye Afisa Mawasiliano na Masoko wa Chuo hicho, Bi. Suzana Magobeko ametoa wito kwa wahitimu wa kidato cha Sita mwaka 2023, wahitimu wa miaka iliyopita na wadau wengine wote kufika katika Banda la SUA na kwamba, wamejipanga vizuri kuwahudumia na kuwapatia ushauri ulio bora utakao wawezesha kufanya maamuzi sahihi katika fani wanazotaka kusoma.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kimeshiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi, hususani wanafunzi kukutana na wataalamu wao waliobobea katika fani mbalimbali ili kutambua fursa zilizopo katika Chuo hicho, sambamba na kufanya Udahili wa Papo kwa hapo.

Aidha katika maonesho hayo zaidi ya wananchi 3600 waliotembelea Banda la Chuo hicho wamesajiliwa katika ngazi mbalimbali ikiwemo astashahada, Stashahada, Shahada za awali na Shahada za Uzamili.

Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo, “Kukuza ujuzi nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa uchumi imara na shindani” yameshirikisha Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu zaidi ya 80 ambapo, yanatarajiwa kuhitimishwa rasmi Julai 22, Mwaka huu.

Previous articleWAJUMBE BODI YA USHAURI BRELA WAPIGWA MSASA
Next articleYAJAYO YANAFURAHISHA KUPITIA DP WORLD-MJEMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here