Home SPORTS SIMBA KUANZIA RAUNDI YA PILI, YANGA KUIVAA DJIBOUTI

SIMBA KUANZIA RAUNDI YA PILI, YANGA KUIVAA DJIBOUTI

DROO ya Raundi za awali za michuano ya klabu imepangwa makao ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Jijini Cairo nchini Misri na mabingwa wa Tanzania, Yanga wataanza na Asas ya Djibouti.

Hata hivyo Yanga wakifanikiwa kuitoa timu hiyo ya Djibouti, Yanga SC watakutana na mshindi wa jumla kati ya kati ya Otoho ya Kongo Brazzaville na El Mereikh ya Sudan kuwania tiketi ya makundi.

Katika Kombe la Shirikisho, Singida Big Stars wataanza na JKU ya Zanzibar, huku Azam FC wakimenyana na Bahir Dar ya Ethiopia.

Azam FC ikifuzu itamenyana na Club Africain ya Tunisia, wakati Singida Fountain Gate ikipita itakutana na Future ya Misri.

Pia Simba SC itaanzia Raundi ya Pili ya mchujo moja kwa moja kuwania kuingia hatua ya makundi kwa kumenyana na mshindi kati ya African Stars ya Namibia na Power Dynamos ya Zambia ambayo watacheza nayo kwenye Simba Day.

Huku kwa upande mabingwa wa Zanzibar, KMKM watamenyana na St George ya Ethiopia, mtihani ambao ikiuvuka itakutana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.

Katika Kombe la Shirikisho, Singida Big Stars wataanza na JKU ya Zanzibar, huku Azam FC wakimenyana na Bahir Dar ya Ethiopia.

Azam FC ikifuzu itamenyana na Club Africain ya Tunisia, wakati Singida Fountain Gate ikipita itakutana na Future ya Misri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here