Home BUSINESS PURA YAFANYA UTAFITI WA GESI NA MAFUTA BAHARI 

PURA YAFANYA UTAFITI WA GESI NA MAFUTA BAHARI 

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Neema Adriano, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya udhibiti wa Mkondo wa Juu (PURA) inafanya utafiti wa upatikanaji wa nishati ya gesi na mafuta ambayo yanapatikana baharini.

Hayo yamesemwa Juni 5,2023 na Mkurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa mkondo wa juu (PURA) Mhandisi Charles Kamweni wakati wa maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), katika viwanja vya Mwalimu Juliaus Nyerere Jijini Dar es Salaam.,

Amesema, sasa wana mradi mkubwa unatekelezwa hapa nchini ambao ni madini gesi waliyoyagundua maeneo ya bahari kuu  yenye hali ya kimiminika. kwa upande wa mafuta au gesi inayotoka ardhini ukiwa na zao lingine kwa upande wa mafuta unapata mafuta topetope ambalo hilo tope huwa linapelekwa kwenye refinalary na kuchakata na kuchambua mazao mbalimbali kutokana na utofauti wa joto

Ameendelea kusema kuwa Huwa yanachakatwa kupitia mnara mrefu ambao unatoa mazao tofauti tofauti na huwa unakuwa mrefu kwenda juu lakini jinsi inavyopanda juu joto linazidi kupungua.

“Kwa hiyo ukiingiza lile tope Yale mazao ambayo ni rahisi kuyeyuka wakati yakichemka huwa yanabadilika kuwa gesi na yanaendelea kupanda juu Sasa lile tope ambalo mara nyingi linabaki kuwa hivyo na baadaye yanatumika kutengeneza rami lakini juu yake huwa yanatoka mafuta mazito,na juu yake kidogo hayo mafuta mazito yanatoka mafuta ya viwandani,na juu yake inakuja mafuta ya dizeli ya kwenye magari na juu yake yanatoka mafuta ya taa,na juu yake inatola petroli.

“Zile gesi ambazo hazijabadilika huwa zinachukuliwa zinaenda kupozwa kwenye plant ambayo hydrogen zinatoa kitu kinaitwa LPG hiyo ndio gesi ya kwenye mitungi ni mzao wa uchakataji wa mafuta au mafuta ghafi au mafuta mazito,” amesema Kamweni.

Hivyo basi amewaomba Watanzania wote waweze kutembelea Banda lao kuja kupata elimu na kujua yale ambayo wanayafanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here