Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila, akifafanua jambo kwa Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Malipo kutoka Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bw. Nestory Maro, alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano BoT, Bi. Victoria Msina, Mkurugenzi wa Usimamizi Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Kened Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya mikopo ya nyumba (First Housing Finance) Bw. Sasa Chonza pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), Bw. Oscar Mgaya (wa pili kutoka kulia).
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila, akielezea jambo kwa Afisa Utawala Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Suleiman Tajiri, alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano BoT, Bi. Victoria Msina, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), Bw. Oscar Mgaya pamoja ma Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya mikopo ya nyumba (First Housing Finance), Bw. Sasa Chonza (kulia).
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), Bw. Oscar Mgaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya mikopo ya nyumba (First Housing Finance), Bw. Sasa Chonza (katikati).