Home BUSINESS MWANAFUNZI VETA ATENGENEZA MFUMO WA KUZALISHA UMEME WA MAJI

MWANAFUNZI VETA ATENGENEZA MFUMO WA KUZALISHA UMEME WA MAJI

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

Vijana wanaosoma katika Chuo cha VETA Dodoma wameendelea kunufaika na programu mbalimbali za mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho ikiwemo fani ya umeme.

Mmoja wa mnufaika ambaye ni mwanafunzi wa ngazi ya pili katika fani ya umeme katika Chuo hicho,  Patrick Ezekiel Patrick,  ameelezea namna alivyonufaika na mafunzo katika fani ya umeme ambapo kwa kushirikiana na mwalimu wake ameweza kuunda mfumo wa uzalizashaji umeme unaotumia Maji.

“Mfumo huu niliutengeneza kwa kushirikiana na Mwalimu wangu  kunisaidia kuweza kujifunza kwa urahisi jinsi umeme unavyozalishwa, na namna unavyosafirishwa hadi kufika vituo vya kupozea umeme, na kisha kusambaza kwa watumiaji.

“Katika mfumo huu, kunakuwa na Jenereta ambayo litategemea kupata nguvu ya mzunguko kutokana na Kasi ya maji, na pia kutakuwa na Transfoma kwa ajili ya kuukuza umeme.  Pia kunakuwa na vifaa kwa ajili ya kulinda Soketi na vifaa vingine vinavyohitajika kuwepo kwenye Transfoma.

Ameongeza kuwa Mfumo huo ni halisi unaoendana na ule unaotumika katika vituo mbalimbali vya kuzalisha umeme unaotokana na maji hapa nchini.

amewaasa vijana kuacha dhana potofu kuhusu VETA kwani ni chuo ambacho kinatoa mafunzo mbalimbali yatakayopelekea kuwa na ujuzi mkubwa watakaoutumia katika kusaidia jamii kwa utatuzi wa changamoto mbalimbali.

VETA inaahiriki Katika maonesho ya Sabasaba mwaka huu, ikiwa na  wataalamu wao mbalimbali waliofika kutoa elimu na kuonesha kazi wanazofanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here