Home LOCAL MSD YASHAURIWA KUENDELEZA MIKAKATI UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA AFYA

MSD YASHAURIWA KUENDELEZA MIKAKATI UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA AFYA

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Pwani (RAS), Bi. Salvera Salvatory ameishauri Bohari ya Dawa (MSD) kuwa na mikakati endelevu ya kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya ili kuondoa malalamiko kwa wananchi ambayo kwa kiasi kikibwa yameanza kupungua.

Bi Salvatory ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa MSD Kanda ya Dar es Salaam na wadau wake wa mkoa wa Pwani uliofanyika Kibaha.

“Wananchi wanafarijika sana wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakapatiwa Dawa zote walizoandikiwa”

Kiongozi huyo amekiri kuvutiwa na MSD kuwa na kitengo cha Huduma kwa Wateja, ambao ndio hufanya mawasiliano kwa karibu na wadau na wateja, ambapo amewashauri kuhakikisha wanafuatilia malalamiko ya wateja na kufuatilia namna yanavyoshughulikiwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Miradi wa MSD Victor Sungusia ameeleza kuwa usambazaji wa bidhaa za afya mara sita kwa mwaka umesaidia kuongeza hali ya upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya MSD Betia Kaema ameahidi kufanyia kazi maazimio yote yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho huku akisisitiza ushirikiano na mawasiliano ya mara kwa mara na wadau hao.

Previous articleMSAMA AWAASA WABUNGE, VIONGOZI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA
Next articleGGML YAELIMISHA WADAU UTEKELEZAJI MPANGO WA CSR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here