Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Simon Faida (24) mkazi wa kijiji cha Msasa kata ya Busanda mkoani Geita kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 baada ya kumrubuni kwa kumpa vizwadi vidogovidogo ikiwemo kumnunulia chapati.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Geita kamishna msaidizi wa polisi ACP Adamu Maro amesema Mpaka sasa Jeshi hilo linamshikiria mtuhumiwa huyo baada ya vipimo vya dakitari kuthibitsha mtoto huyo kwamba kabakwa na kulawitiwa ambapo mtuhumiwa huyo ambae ni kinyozi wa nywele alitumia mwanya huo kumlubuni mtoto huyo kisha kumbuka na kumlawiti.
“ushahidi wa dakitari tayari umeshatoka na tayari tumeita mshahidi kadhaa kuweza kuwahoji walichoona, walichoshuhudia sasa hivi jarada limeshakamilika na litapelekwa kwa mwanasheria na taratibu za kumpeleka mahakamani ziweze kukamilika mara moja”
Bila shaka huyu alimrubuni mtoto huyo kwa vizawadi vidogvidogo chukua elfu mbili,chukua elf ngapi ukale mihogo au chapati na hatimae akapata nafasi ya kumuingilia
Kamanda Maro ametumia nafasi hiyo kukemea vitendo hivyo pamoja na kuwataka wanafunzi kuwaepuka wanaume wanaowarubuni kwa lifti,fedha na zawadi ndogo ndogo ili kuepuka vitendo vya ukatili kwa jamii.
Swahili Times imepata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya kalangalala ambao wamelaani vikali kitendo alichofanyiwa mwanafunzi huyo huku wakiiomba serkali kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaume wale wote wanaobainika kufanya ubakaji ili kuweza kukomesha vitendo hivyo.