Home LOCAL RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA JOPO LA WAZEE WA...

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA JOPO LA WAZEE WA SADC

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Spika wa Bunge la Lesotho; Mhe. Mamonaheng Mokitimi. 

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yuko katika Ufalme wa Lesotho kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Jopo hili la Wazee wa SADC ambalo Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Paramasivum Pillay B. Vyapoory, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius, limekutana na Serikali na wadau mbalimbali ndani ya Ufalme wa Lesotho, kama mwendelezo wa juhudi ya kusaidia upatitanaji wa utulivu wa kisiasa katika Ufalme huo.

Jopo limekutana na Mhe. Ntsokoane Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho; Mhe. Nthomeng Justina Majara, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge; Mhe. Tlohang Sekhamane, Spika wa Bunge la Lesotho; Mhe. Mamonaheng Mokitimi, Mwenyekiti wa Seneti; Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Viongozi wa Vyama vya Upinzani; Uongozi wa Ofisi ya Mpito ya Mabadiliko ya Kitaifa (NRTO); Viongozi wa Umoja wa Machifu; na wadau mbalimbali.

Previous articleFANYENI KAZI KWA WELEDI KWA KUZINGATIA MAADILI -SENYAMULE 
Next articleKINYOZI MBALONI TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 8 GEITA KWA KUMHONGA CHAPATI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here