Home BUSINESS KATIBU MKUU MADINI ATEMBELEA BANDA LA GGML SABASABA, AKOSHWA NA REKODI YA...

KATIBU MKUU MADINI ATEMBELEA BANDA LA GGML SABASABA, AKOSHWA NA REKODI YA KAMPUNI HIYO

Meneja Usalama kazini kutoka GGML, Isack Senya (wa pili kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba namna Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited ilivyoweka rekodi ya kunyakua tuzo ya kimataifa kwenye masuala ya usalama kazini (Global Safety Awards).

 Afisa Uhusiano wa Jamii  kutoka GGML, Doreen Dennis  (wa pili kulia) akimuelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Magogo – Geita utakaokuwa uwanja wa nyumbani wa Klabu ya Geita Gold Football Club inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Mradi huu wa kijamii unafadhiliwa na AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited. Kulia ni Afisa Mwandamizi (Rasilimali Watu), Innocent Mushi.

KATIBU mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Felchesmi Mramba ametembelea banda la Maonesho la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam, na kushuhudia rekodi za kipekee zilizowekwa na kampuni hiyo kutoka mkoani Geita.

Katika maonesho hayo, GGML inajivunia kushiriki kwa mara nyingine tena huku ikiwa imenyakua tuzo ya Kimataifa ya masuala ya Usalama kazini (Global Safety Awards) pamoja na utekelezaji wa miradi kemkem ya inayoinufaisha jamii ya Watanzania.

Maonesho ya Saba Saba ambayo ni fursa kwa Tanzania kushuhudia matunda ya mafanikio yaliyotekelezwa katika nyanja mbalimbali pia yanatajwa kuwa fursa ya kusherehekea maendeleo ya sasa na kuangalia malengo ya taifa ya baadae. 

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JULAI 6 -2023
Next articleNAIBU GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA DKT. YAMUNGU ATEMBELEA MABANDA MAONESHO YA SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here