Home LOCAL JAJI MKUU ASHIRIKI IBADA YA MKE ALIYEKUWA JAJI MKUU WA KWANZA MTANZANIA

JAJI MKUU ASHIRIKI IBADA YA MKE ALIYEKUWA JAJI MKUU WA KWANZA MTANZANIA

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mke wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi, marehemu Bi. Elizabeth Augustine Saidi, katika katika Kanisa la Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Petro (St. Peters), Osterbay, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 26, Julai 2023 wakati ibada ya kuuaga.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma  akitoa hotuba yake katika ibada hiyo.

Jaji Mkuu Msaafu, Mhe. Barnabas Samatta akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mke wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi, marehemu Bi. Elizabeth Augustine Saidi, katika katika Kanisa la Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Petro (St. Peters), Osterbay, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 26, Julai 2023 wakati ibada ya kuuaga.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na (kulia)na Jaji Mkuu Msaafu, Mhe. Barnabas Samatta(kushoto) wakifuatilia ibada.

 Familia ya marehemu ikiwa ibadani.

(Picha naMagreth Kinabo- Mahakama)

Na: Magreth Kinabo -Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 26 Julai, 2023 amewaongoza mamia ya waombolezaji katika ibada ya kuuaga mwili wa mke wa  aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi, Bi. Elizabeth Augustine Saidi, ambapo amesema atakumbukwa kwa ucheshi wake na kuuliza maswali kama Jaji.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Petro (St. Peters), Osterbay, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 9 alasiri ikiongozwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Padre Alista Makubi.

Akimzungumzia marehemu Jaji Mkuu, Prof. Juma amesema ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake, alikuwa ni mcheshi na muuliza maswali kama majaji.

“Mara ya kwanza nilikutana naye tarehe 30 Mei, 2023 nyumbani kwake Mtaa wa Augustine Saidi, alikuwa na maswali kama Jaji, mke wa Jaji Mkuu uiga stahili za Majaji, anasema Mhe. Jaji Mkuu Prof. Juma. 

Mhe, Jaji Mkuu ameongeza kuwa anakumbuka  swali aliloulizwa na marehemu kuwa Je wewe unakalia kiti alichokalia mume wangu? Ambapo alimjibu ndio hali iliyosababisha vicheko, furaha na utani katika mazungumzo yao.

Aidha Jaji Mkuu amesema kwamba marehemu na mumewe wameacha historia katika vitabu vya Mahakama ya Tanzania.

Naye mjukuu wa marehemu, Anitha Bulindi akisoma wasifu wa bibi yake amesema watamkumbuka kwa upendo aliouonesha kwa familia, kutoa ushauri na kuwaimbia nyimbo za upendo, kuwajali yatima, majirani  na ucha Mungu.

Kwa upande wake Padre Paschal Kamugisha amewataka waombelezaji kuishi katika imani na mafundisho kama alivyokuwa marehemu, kusali kwa bidi, kutenda matendo ya huruma.

“Tutamkumbuka kwa jinsi aliyojitolea kutoa mazao ya shamba kwa watumishi wa Mungu. Mama wa Kanisa,” amesisitiza.

Ibada hiyo imehudhuria na Jaji Mkuu Msaafu, Mhe. Barnabas Samatta, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Thomas Mihayo, mke wa Jaji Mkuu, Mama Marina Juma, wakiwemo baadhi ya wenza wa Majaji.

Marehemu Bi. Elizabeth   alizaliwa tarehe 29 Agosti 1937 na alifariki dunia tarehe 21Julai, 2023 ghafla jijini Dar es Salaam. Mazishi ya Mama Elizabeth yatafanyika kesho Alhamisi tarehe 27 Julai, 2023 nyumbani kwake Nduweni Marangu, Moshi.

Marehemu Jaji Saidi aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu mwaka 1971 hadi 1977 baada ya mtangulizi wake Mzungu, Philip Telford Georges kuerejea kwao Trinidad and Tobago aliyekuwa Jaji Mkuu tangu mwaka 1965. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here