Home BUSINESS GGML YAELIMISHA WADAU UTEKELEZAJI MPANGO WA CSR

GGML YAELIMISHA WADAU UTEKELEZAJI MPANGO WA CSR

MAONESHO ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, yanayofanyika katika viwanja vya SabaSaba, yamekuwa ni fursa adhimu kwa wadau mbalimbali kushuhudia namna kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) inatekeleza Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Moja ya wadau hao ni Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse ambaye juzi Jumanne tarehe 4 Julai 2023 ametembelea banda la GGML katika maonesho hayo  yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Dk. Mwasse alipata maelezo kutoka kwa Afisa Manunuzi (Mikataba) wa GGML, Silas Shija (wa kwanza kulia) aliyekuwa ameambatana na Scholastica Hoya, Ofisa Rasilimali Watu na Innocent Mushi ambaye ni Ofisa Mwandamizi (Rasilimali Watu).
Walieleza jinsi GGML inavyosaidia miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika jamii zinazozunguka migodi yake kama vile elimu, afya, maji, miundombinu na kilimo.
Miradi hii inaakisi dhamira ya GGML kwa jamii inayozunguka mgodi kuwa na maendeleo endelevu.
Mojawapo ya maadili yake ya msingi, na maono yake ni kutoa mchango chanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here