Home BUSINESS CHUO CHA BAHARI (DMI) CHAPATA MWITIKIO MKUBWA KWA WANANCHI SABASABA

CHUO CHA BAHARI (DMI) CHAPATA MWITIKIO MKUBWA KWA WANANCHI SABASABA

Makamu Mkuu wa Chuo cha DMI, Fedha Utawala na Mipango, Dkt. Wilfred Kileo akiwafafanulia wageni Kozi zinazotolewa chuoni Kwa wageni waliotembelea Banda la Chuo kwenye maonesho ya sabasaba

Kaimu Msajili wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam Mr. Benard Mgendwa akimsajili mteja aliyefika kwenye Banda la Chuo kwenye maonesho ya sabasaba.

Afisa habari wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam Edwin Ekoni akifafanua Kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni na namna ya kujisajili online Kwa Mgeni aliyetembelea Banda la Chuo kwenye maonesho ya sabasaba.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM 

Wananchi mbalimbali hususani vijana wanaotaka kusomea fani za Bahari wameendelea kujitokeza kwa wingi katika Banda la Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kujiunga na fani mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho.

Akizungumza katika Mahojiano na waandishi wa habari Julai 12, 2023 katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Udahili wa Chuo hicho Bw. Bernard Mgendwa, amesema kumekupo na mwitikio mkubwa wa vijana kujitokeza kujiunga na chuo hicho katika fani mbalimbali ikiwemo ya Ubaharia.

Ameeleza kuwa Chuo hicho kimeshiriki maonesho kueleza shughuli za kitaaluma na fursa zitokanazo na Uchumi wa Buluu kupitia Bahari, Mito na Maziwa iliyopo nchini

“Dirisha la Udahili kwa awamu ya kwanza lilifunguliwa Mei 16, na litafungwa Julai 30 Mwaka huu kwa wanaojiunga na masomo ngazi ya Cheti, Stashahada, pamoja na Shahada za Udhamili.

“Awamu ya Pili ilifunguliwa Juni 16 na Dirisha hilo litafungwa rasmi Agosti 4 mwaka huu kwa ngazi ya Shahada pekee, hivyo wanafunzi wanaotaka kujiunga wanahimizwa kuzingatia kalenda ya Udahili kabla Dirisha halijafungwa” ameeleza Bw. Mgendwa.

Aidha ameongeza kuwa, Chuo hicho kinatoa kozi  na programu mbalimbali za Bahari kwa watu binafsi, pamoja  na nchi mbalimbali za jirani ikiwemo, Kenya, Uganda, Komoro, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo na Namibia.

Aidha, DMI inatambulika kwa programu zake za mafunzo ya ubora wa hali ya juu katika tasnia ya Bahari kwa kufuata viwango vya kimataifa.

Ametoa mwito kwa wananchi na watu wote kuendelea kujiunga na Chuo hicho mahali popote walipo ambapo wanaweza kujisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Chuo www.osim.dmi.ac.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here