Home BUSINESS ACB BENKI KUJIKITA KULETA MAPINDUZI YA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

ACB BENKI KUJIKITA KULETA MAPINDUZI YA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

Na:  Mwandishi wetu

Akiba Commercial Bank Plc( ACB) imesema itahakikisha inaendelea kujikita kuleta mapinduzi ya utoaji huduma bora za kibenki hapa nchini kwa kuboresha huduma zake ikiwemo kuweka fedha na kutoa fedha pia kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa .

Akizungumaza Jijini Dar es salaam na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi wakati katika banda la benki hiyo katoka maonyesho ya ya 47 ya Sabasaba ndani ya amesema kuwa benki ya Akiba imeboresha huduma zake ambazo zitakuwa chachu ya kukidhi matarajio ya wateja waliopo pamoja na wateja watarajiwa katika kujipatia huduma.

Hata hivyo amebainisha kuwa Maboresho makubwa yamefanywa kwa huduma za wateja binafsi,(Personal banking) ambayo inawalenga Waajiriwa wa sekta za Umma na sekta binafsi ambapo mteja anaweza kupata mikopo ya aina mbalimbali kuendana na mahitaji yake mathalani huduma za mikopo ya kujenga na kuboresha makazi, pia mikopo ya muda mfupi (Salary advance) kwa ajili ya kutatua dharura za kifedha kwa muda mfupi. 

” Benki imezidi kuboresha huduma za mikopo kwa wateja wakubwa ,w (Corporate customers) wakati,na wadogo kuendana na mahitaji ya soko na tunatoa huduma za bima kwa wajasiriamali pamoja na vikundi mbalimbali ikiwemo mikopo ya bima –IPF (Insurance Premium Financing)” amesema Mkurugenzi

Sambamba na hayo Mkurugenzi amebainisha kuwa benki imeboresha huduma zake kwa kupitia Mawakala wake (Akiba Wakala) na simu ya mkononi (Akiba Mobile) pia imeboresha mifumo ya utumaji pesa kwenda nje ya nchi.

Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo na amewashukuru kuchagua benki ACB hiyo kutumia huduma zake ikiwemo wafanyakazi ,Wajasriamali hivyo amewasisitiza waendelee kupata huduma bora kwani ni benki sahihi na bora inayolenga kutimiza malengo ya Wateja wake.

Previous articleCHUO CHA BAHARI (DMI) CHAPATA MWITIKIO MKUBWA KWA WANANCHI SABASABA
Next articleEPSON YAFUNGUA KITUO CHA KWANZA CHA MAUZO NA HUDUMA YA ZIADA AFRIKA MASHARIKI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here