Home BUSINESS BRELA YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA BUGURUNI

BRELA YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA BUGURUNI

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewahimiza wafanyabiashara katika eneo la Buguruni, Wilaya ya Ilala, kurasimisha biashara zao ili kuwa na utofauti kati ya biashara moja na nyingine.

Wito huo umetolewa leo tarehe 26 Julai, 2023 na Afisa Usajii wa BRELA Bw. Yusuf Mwasakafyuka wakati wa ukaguzi elimishi kwa wafanyabiashara waliokuwa wakipata elimu kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani.

Akizungumza na wafanyabiashara hao Bw. Mwasakafyuka amesema zoezi hilo limelenga katika kutoa elimu na kuhimiza kuhusu umuhimu wa kurasimisha biashara.

“Lengo kuu ni kuwapa elimu wafanyabiashara ambao bado hawajasajili biashara zao na wale ambao tayari wamesajili ili watekeleze matakwa ya kisheria baada ya usajili”, amesema Bw. Mwasakafyuka.

Pia ametumia fursa hiyo kuwasikiliza na kupokea changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kupata huduma za BRELA kupitia mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao .

Ukaguzi huu elimishi utaendelea kufanyika katika wilaya zote za Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni.

Previous articleSERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WENYE VIWANDA – DKT. KIJAJI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JULAI 27,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here