Home LOCAL WRIKALI YA TANZANIA , UBALOZI WA ITALIA KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA ZA RITA

WRIKALI YA TANZANIA , UBALOZI WA ITALIA KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA ZA RITA

Na: Sophia kingimali, DA RE SALAAM

Serikali ya Tanzania Kwa kushirikiana na ubarozi wa Italy wametiliani saina ya mkataba wa msaada Kwa ajili ya kuboresha huduma Kwa wakala wa usajili,uzamini na ufilisi Rita ili kuboresha huduma zake…

Akizungumza Leo June 23,2023 mwenyekiti wa bodi Dtk Amina Msengwa amesema msaada huo walioopokea utasaidia katika usajili wa watoto walio chini ya miaka.

Aidha Dkt Msengwa amesema kuwa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa utaanzia kuanzia ngazi ya mtaa ambapo mtu anaweza kuomba cheti na kupatiwa..

“Msaada huu utasaidia kuboresha huduma za usajili wa watoto chini ya miaka mitano kuanzia ngazi za mtaa lakini pia unaweza huduma ya cheti kupitia mtandao wa erita hii ni Kwa ajili ya watu wote”ameongeza Msengwa.

Nae katibu mkuu wizara ya Fedha Dkt Natu Mwamba amesema kuwa wamepokea msaada huo wa bilioni Moja Kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa Takimu wa usajili wa raia hapa nchini ambapo watoto 348391 watanufaika na usajili huo utakaofanyika Katika wilaya 11 za mkoa wa Tanga.

“Msaada huu utawawezesha rita kutekeleza usajili wa raia na takwimu muhimu Kwa ugatuzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika kata 245 na vituo vya Afya 405 katika mkoa wa Tanga”amesema Mwamba

Kwa upande wake barozi wa Itali nchini Marco Lombard amesema wataendelea kusaidiana na serikali katika kuhakikisha uchumi wa nchi na maendeleo yanapatikana Kwa wananchi pamoja na kuboresha huduma katika sekta mbalimbali.

“Tumesaini mkataba huu wa kusaidia mradi wa usajili wa wakala wa usajili,ufilisi na udhamini (RITA) lengo letu ni kuisapoti serikali ya mama Samia ili kazi iendelee”amesema Lombordi

Mkataba uliosainiwa ni mkataba wa msaada ili kuboresha huduma za usajili Rita ambapo zitajikita katika mkoa wa Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here