Home LOCAL KINANA NA JAKAYA WASHIRIKI UFUNGUZI WA MSIKITI WA TAQWA MTAKANINI, WILAYA YA...

KINANA NA JAKAYA WASHIRIKI UFUNGUZI WA MSIKITI WA TAQWA MTAKANINI, WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI KATAVI

Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Ally bin Muhidin Mkoyokole akifungua Jiwe la Uzinduzi Rasmi wa Msikiti wa Taqwa Mtakanini Uliojengwa na Mwananchi na Mkazi wa Kijiji hicho Ndg. Ramia Yasin.

Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Ally bin Muhidin Mkoyokole(Mwenyekitambaa begani)  akikata Utepe kuashiria Uzinduzi Rasmi wa Msikiti wa Taqwa Mtakanini Uliojengwa na Mwananchi na Mkazi wa Kijiji hicho Ndg. Ramia Yasin.
Rais Mstaafu wa Awamu ya NNE Mhe Jakaya Mrisho Kikwete Akizungumza  katika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Taqwa katika kijiji cha Mtakanini Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma .
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza katika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Taqwa katika kijiji cha Mtakanini Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Rais Mstaafu wa Awamu ya NNE Mhe Jakaya Mrisho Kikwete Akizungumza na Kufurahia jambo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman Kinana katika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Taqwa katika kijiji cha Mtakanini Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Wananchi Mbalimbali pamoja na Viongozi waliohudhuria  katika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Taqwa katika kijiji cha Mtakanini Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya NNE Mhe Jakaya Mrisho Kikwete wakikagua Muonekano wa Ujenzi wa Msikiti wa Taqwa Mtakanini.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Komred Abdulrahman Kinana,Akisalimia Wananchi alipowasili katika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Taqwa katika kijiji cha Mtakanini Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Komred Abdulrahman Kinana Akiwa na Viongozi wa Mkoa wa Songea wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM (Mwenye Koti la rangi ya kijivu) Ndg. Odo Mwisho, mara baada ya Kuwasili katika Uwanja Wa Ndege Mkoani humo.

Rais Mstaafu wa Awamu ya NNe Mhe Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameambatana na Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Ally bin Muhidin Mkoyokole (Kushoto) , Ndg. Ramia Yasin Mwananchi na Mkazi wa Kijiji Cha Mtakanini aliyejenga Msikiti huo,pamoja na Viongozi Mbalimbali mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Msikiti Huo.(PICHA ZOTE NA Fahadi Siraji)
Previous articleKATIBU MKUU CCM ASEMA WATAENDELEA KULINDA WAZALISHAJI MBOLEA WA NDANI
Next articleWRIKALI YA TANZANIA , UBALOZI WA ITALIA KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA ZA RITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea KINANA NA JAKAYA WASHIRIKI UFUNGUZI WA MSIKITI WA TAQWA MTAKANINI, WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI KATAVI