Home BUSINESS WANAWAKE SOKO LA BATIKI MCHIKICHINI WATOA KILIO KWA RAIS SAMIA

WANAWAKE SOKO LA BATIKI MCHIKICHINI WATOA KILIO KWA RAIS SAMIA

Na Heri Shaaban (Ilala)

Umoja Wanawake wa kutengeza batiki soko la Mchikichini wametoa kilio chao kikubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,wa Wanawake wa soko hilo mikopo ya Halmashauri imewapitia pembeni hivyo kupelekea kukosa mitaji ya Biashara .

Umoja wa Wanawake wa soko la Mchikichini (KIUWASO )walisema hayo katika mafunzo iliyoandaliwà na Umoja huo wa Wanawake wa Batiki Mchikichini kwa kushirikiana na Benki ya Azania ambao walikuwa wakitoa Elimu ya mikopo .

Akizungumza katika mafunzo hayo Katibu wa Wanawake wa soko la Mchikichini Adela Raymond Swai, alisema umoja wanawake wa Batiki wa soko la Mchikichini mikopo ya Serikali imewapitia nyuma hivyo ulazimika kutafuta njia ya ziada waweze kupata mitaji

“Tunaomba Serikali yetu sikivu inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan isikie kilio chetu Umoja wanawake wa Batiki wa soko la Mchikichini tuwezeshwe mikopo ya Serikali tuweze kukuza mitaji yetu ya biashara katika soko letu tumekuwa tukifatilia mikopo ya Halmashauri bila mafanikio “ alisema Adela.

Adela alisema Batiki zote utakaziona ,Kenya ,Uganda ,na nchi za Afrika zote zinazalishwa na Umoja wanawake wa Mchikichini Wilayani Ilala .

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wanawake Mchikichini Elnaike Kimati alisema changamoto kubwa katika umoja wao vitendea kazi wanatumia moto wakati wote wanaomba serikali iwatazame kwa jicho la Karibu ,ambapo toka soko hilo liungue wameathitika ukosefu wa mitaji pamoja na Bima wengi hawana wakiunguliwa wanajenga wenyewe kwa pesa zao

Makamu Mwenyekiti Kimati aliomba Serikali kupitia Waziri wa Biashara kuwatafutia fursa na masoko ya nje Ili waweze kukitangaza zaidi pamoja na nchi yetu .

Mwisho.

Previous articleGGML YATOA ELIMU YA HAKI, WAJIBU MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA 
Next articleWATAKA TEHAMA ISIATHIRI MALEZI, HAKI ZA WATOTO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here